MWIGULU NCHEMBA AANZA KWA KUTOA ONYO KALI KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA




Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka
wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja
biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.

Waziri Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua
kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.

Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na
Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na
utulivu katika nchi.

Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa
atahakikisha anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake
ili kufanya mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya
Watanzania.

Pia Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia
changamoto zinazozokabili vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi
vizuri katika miaka ya hivi karibuni.

Mawaziri walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo
na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.

Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza
nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh. Charles Kitwanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli,akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwiguli Nchemba mara baada ya kumwapisha leo Ikulu Jijini Dar es salaam.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post