Mwenyekiti wa
Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimkabidhi kadi ya uanachama
Goodluck Ole Medeye aliyekuwa mwanachama wa chama cha Demokrasia CHADEMA .
Na Woinde Shizza , Arusha
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi( UVCCM) umetabiri
ipo idadi kubwa ya wanachama hasa vijana waliokumbwa na gharika ya
kumfuata Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuhamia Chadema
watakihama chama hicho kwasababu si taasisi kamili ya kisiasa ila ni
kijiwe cha wasaka madaraka na vyeo .
Pia Umoja huo umesisitiza kuwa kuanza kuhama kwa Waziri
zamani Goodlucky Ole Medeye ni mwanzo wa matayarisho ya vigogo wengine
zaidi waliohamia chadema bila kukipima na kukipekua kiundani
watajiondoa wakati wowote baada ya kuisoma namba.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengai ole Sabaya
ameeleza hayo jana wakati akizungumza wana wanachama wapya wa UVCCM na
kuzindua shina jipya la wakereketwa katika kijiji cha Obalbal wilayani
Ngorongoro Mkoani hapa.
Sabaya alisema kosa walilofanya baadhi ya viongozi na
wanachama maslahi kuihama CCM kwa tashtit na mbwembwe anaamini kuwa siku
zao sasa zinahesabika na wako njiani kujiondoa chadema huku baadhi yao
wakitamani kurudi CCM ila milango ya kuingilia imefungwa kwa kuzuia
usaliti na uasi .
Mwenyekiti huyo alifika katika kijiji cha Olbalbal
kufuatilia iwapo wananchi katika kijiji hicho walipelekewa na serikali
msaada wa mahindi ya chakula na kuwatosheleza.
Akizungumzia wanachama waliofuata mkumbo kwenda Chadema,
alidai walifanya maamuzi ambayo si ya kizalendo , hayakutokana na
tashwishi ya ukomavu wa imani yankisiasa wala kiitikadi ila walijikuta
wakimfuata mtu kwa matumaini ya kupata na sasa wamejikuta wakipatikaana .
"Kuingia chama lazima mwanachama uwe na imani ya chama
husika, sera zake, itiakadi na miongozo yake, waliokwenda Chadema hivi
wamevutiwa na jambo lipi, mikuusanyiko, kuvaa magwanda au kusema mwaka
huu hadi kitaeleweka" alihoji Sabaya.
Hata hivvo Mwenyekiti huyo aliwaeleza vijana katika kijiji
hicho na kuwashitakia kwa wazazi wao kwamba wake na vijana wao
wawaeleze kuwa maana ya kushika madaraka na kuongoza utawala ni lazima
wapatikane viongizi wenye busara, hekima, maono, kipaji na uwezo wa
kuiweka pamoja jamii bila mifarakano na migawanyiko.
Sabaya akisema iwapo vitu hivyo angepungukiwa navyo au
mungu kutomjaalia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Ali Hassan
Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dk Jakaya kikwete ,Taifa letu lisingepata
sifa kimataifa ya kuwa ni tulivu , lenye umoja na ustawi wa amani.
Alisisitiza kuwa kwakuwa viongozi hao wote wamebahatika
kuwa na upeo, maarifa na hekima ya kuzipima, kupembua na kutambua
mabadiliko ya nyakati huku wakiwa na nia njema ndiyo maana waliiongoza
Taifa kwa kufuata miiko, sera na maelekezo ya chama chao .
Alisema kuwa wale wote Waliopeperushwa na upepo wa
kimbunga cha Lowassa kwanza wa subiri mpaka wao wajiridhishe kama
bado ni wale wale au wamelishwa uasi na mioyo yao kama imeshiba
uzalendo wa kutosha.