UVCCM KILIMANJARO WAIWAKIA CHADEMA


Na Mwandishi Wetu,Kilimanjaro
Umoja wa Vijnana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kikimanjarp umelaani vikaki  tukio la fujo na uvunjifu wa amani kulikosibabishwa na ukaidi wa viongozi wa chadema huko Kahama amkoani shinyanga  juzi na kusema siasa za upindaji na upingaji wa sheria na umwqjaji damu za watu zisiruhusiwe nchini.
Aidha  Umoja huo umeleeza kuwa kitendao cha viongozi wa kisiasa kukaidi sheria kwa lengo la kupata umaarufu  hakuonyeshi kama chadema wana viongozi waliopevuka kisiasa na kiutawala ambao wanaonyesha kukosa upeo  wa kubeba dhima na amana ya uongozi wa Taifa.
Hayo yameelezwa  na Mwenyekiti  wa UVCCM Mkoa kilimanjaro Juma Raibu Juma alipozungumza na waandishi  wa habari mjini Moshi  akilaani na kushutumu siasa chafu za Chadema.
Raibu alisema Tanzania na wanachi wake hawako tayari kukiona chama cha siasa aina ya chadema kikifamya siasa za kuitagutia jamii  majanga, maafa na vurugu ambazo mwishowe zitagharimu maisha au uhai wa watu wasio na hatia.
Alissma juhudi za chadema katika mpango wao wa kujaribu kuzima moto wa utendaji ulioanzishwa na Rais Dk John Magufuli hauwezi kuzimika au kuzimwa kwa uitishaji wa mkiutano yabhashara au maandamano ya chadema ambayo aliyaita  hayana ajenda wala sababu za msingi.
"Chadema kama wameona moto wa utendaji wa Dk Magufuli utawafuta katika ramani ya siasa wakubali matokeo kwani hawana mbinu wala ujanja wa kumzuia kiongoao huyo asizidi kukunalima katika jamii, wakiandamana kibabe  sheria zitachukua mkondo wake"alieleza Raibu.
Alisema mataifa yote duniani yanaelewa kuwa Tanzania ni Taifa la aina yake, linaloheshimu mipaka ya kisheria, kufuata msingi ya utawala bora, demojrasia na kulinda haki za binaadamu hata kabla ya kuruhusiwa kwa mgumo wa vyama vingi mwaka 1992. .
Mwenyekiti huyo wa UVCCM Mkoani Kilimanjaro  alisisistiza kuwa Taifa halitakuwa tayari kuhatarisha maisha na usalama wa watu wake milioni 45 kwa ajili ya manufaa ya kikundi cha viongozi wachache ambao husaka madaraka kinyume na taratibu. 
"Taifa letu lina Katiba yake, sheria zake, mfumo na utaratibu wake wa kanuni husika, atakayeheshimu sheria ataheshimiwa na atakayevunja sheria hataachwa bila kushughlikiwa kwa mujibu wa katiba "alisisistiza Mwenyekiti huyo aliyeambatana katika mkutano huo na kada wa CCM  Mkoani hapa Mwanasheria Frank Nkya.
Alissma ikiwa chadema kilishindwa iuoatabuchaguzi wa urais kwa kutukia sera na ilani yao tokea mwaka 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 hakutatokea muujiza kwa chama hicho kipate ushindi kwa maandamano au vurugu kama kinavyofiiiria.
Raib amevitolea wito vyombo dhamana  vya ulinzi wa usalama wa raia mkoani humo kuendelea kusimamia  majukumu na wajibu wao na kutaka vichukue hatua stahili pale inapotokea mtu mmoja, chama cha siasa au kikundi chochote kitakapthubutu kuhatarisha misingi ya amani, utulivu na mshiamano wa kitaifa uliodumu kwa miaka mingj nchini.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post