REGINA:CHADEMA KINASHIDWA SIASA ZA KIUSTAARABU NA UUNGWANA


 
 Na Mwandishi Wetu, Manyara
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) Mkoa wa Manyara umedharau mtindo mpyabwa kuvunja sheria za unaotaka kutumiwa  na chadema na kwamba usipodhibitiwa mapema kisheria na kikatiba unaweza kuhatarisha umoja, amani, utulivu na mshikamano uliopo nchini.
Pia umoja huo umeelezea na luonyesha kusikitishwa  na tabia ya viongozi wa chama hicho kupungukiwa  uungwana wa kisiasa, uwezo wa kujenga nguvu ya hoja ili  kujiimarisha badala yale wakiamua kushabikia  ghasia na fujo za kisiasa.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa  wa Manyara Regina Ndege ameeleza hayo jana  katika mkutano wake  na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya UVCCM wilaya ya Babati  mjini Mkoani hapa.
Regina alisema kwa uzoefu uliopo katika siasa za Afrika na duniani kwa ujumla  kulingana na matukio yote hatarishi  ambayo yamepelekea na kusibabisha kuzuka  machafuko, umwagaji damu, mgawanyiko wa kijamii na mapigano , alieleza  yalianza kama wanavyofanya viongozi  wa chadema huko Kahama Mkoani shinyanga.
Alisema masuala yote ambayo huashiria hali ya kuvunjia kwa mustakabali wa amani ya nchi, usalama wake au tishio la kutetereka  mshikamano, yanapoachwa kwa jicho la kuyapuuza, ghafla  yanaweza kuisambaratisha nchi .
"Haiwezekani mtu ahatarishe amani , umoja wa kitaifa au utulivu uliopo kwa kisingizio  cha demokrasia ya vyama vingi, ulimi wa binadamu unenapo ubaya huwa ni sawa na mtu anayemwaga pipa la petrol  katikati umati wa watu "alisema Regina.
Aidha Mwenyekiti huyo alieleza kuwa kitendo cha viongozi wa kisiasa kuhamasisha wafuasi wao wakaidi amri halali za polisi au kushiriki kuvunja sheria za nchi hakipaswi kuachwa na kutazamwa macho.
"Hawa viongozi wa Chadema wanajaribu kuutikisa mbuyu ili kujua kama wataweza kuung"oa a  la, wakiona vyombo vyenye dhamana vimekaa kimya bila ya kuwashughukiwa watajenga mazoea ya kudhihaki sheria, tunasema wasizoee  hivyo badala yake wadhihitiwe mara moja ili nchi yetu  ibaki salama "alieleza Mwenyekiti huyo wa UVCCM Manyara .
Regina hata hivyo amelipongeza jeshi  hi la polisi kwa kuchukua hatua za haraka na stahiki za kuwakabili wale wote ambao walipania kuleta jeuri na kiburi cha kutoheshimu utii wa sheria na kukiuka misingi ya utawala bora .
Mwenyekiti huyo amekitaka chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) kama kweli kina ubavu na hoja yakinifu kijiandae kwa kushindana na CCM mwaka 2020 iwapo seriakali ya Rais Dk John Magufuli itashindwa kutekeleza yale iliowaahidi wananchi na si kutaka ushindani katika muonekano wa siasa za kitoto.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post