Washiriki wa Shindano la kumsaka mlimbwende katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza la MISS ILEMELA 2016 (pichani), wakionyesha upendo wao kwa 102.5 Lake Fm Mwanza, walipotembelea Kituo cha Utamaduni Bujora kilichopo katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza
Walimbwende hao wamepiga kambi katika hotel ya "New Bujora Point" iliyopo Magu ili kujinoa na fainali za shindano hilo linalotarajiwa kufanyika jumamosi ijayo June 4, 2016 katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza, ambapo kiingilio itakuwa shilingi 10,000 kawaida na shilingi 30,000 kwa VIP huku wasanii mbalimbali wakiongozwa na Ney Wa Mitego wakitarajiwa kudondosha burudani kali.
Pamoja na mambo mengine, lengo la washiriki hao wa shindano la Miss Ilemela 2016 ambao mwaka huu ni 16, ni kutembelea kituo hicho ni kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na utamaduni wa kabila la Kisukuma.