Kwa ufupi Women Charity Group ni kundi
la
wanawake na mabinti wanaomtumikia Mungu
kupitia maombi, kuombea Familia,Taifa
na mambo mengine mengi . Pia hufanya kazi za kujitolea katika maeneo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Ocean Road ambapo walitoa msaada
kwa watu wenye Saratani mwaka 2014, mwaka 2015 walitembelea
Mburahati kwa watoto yatima waishio na masista,
mwaka huu wameweza kwenda Muhimbili kutoa msaada kwa
watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo
wazi.
Wanakikundi
cha Women Charity Group wakiwa wanaingia katika Hospitali ya
Muhimbili pamoja na Baadhi ya vitu vyao walivyokwenda kutoa msaada kwa
watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na migongo
wazi.
Mmoja wa wauguzi
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitoa Shukurani zake baada ya
kupokea msaada huo
Kikundi
cha Women Charity wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa msaada
huo.