Mke wa rais wa wa kwanza wa kenya Mama ngina akipokea zawadi (award) kutoka bunge la jumuiya ya afrika mashariki ikiwa ni kumbukumbu ya mchango uliofanywa na mwanamme wake Jomo kenyata kutoka anaye mkabidhini spika wa bunge la afrika mashariki Daniel Kidega
Mbunge wa bunge la jumuiya ya afrika mashariki Makongoro nyerere akipoa nishani kwa niaba ya mama yake maria nyerere kutoka kwa spika wa bunge hilo ,makongo alipokea nishani hiyo kwa vile mama yake mama maria nyerere akuhuzuria mualiko huo kutokana na kile alichodai kuwa ni mgonjwa na pindi atakapomaliza vikao vya bunge la bajeti lingaloendela atamfikishia
Muonekano
wa bunge la Afrika mashariki likiendelea na shughuli zake kwenye makao
makuu ya bunge hilo jijini Arusha kwa kikao cha bajeti ya jumuiya ya
Afrika mashariki
Na Woinde shizza,Arusha
BUNGE
la Jumuiye ya Afrika Mashariki limemwagiza Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo
ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli
kuwachukulia hatua kali mawaziri wote wanaohusika katika wizara
zihususuzo Jumuiya hiyo kwa kutokuhudhuria vikao vya Bunge hilo.
Pamoja
na hilo pia imebainika kuwa kutokuhudhuria kwao kwenye vikao hivyo ndio
chanzo cha wananchi wa Jumuiya hiyo kutojua mambo mengi yahusuyo
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo yamesemwa kwa masikitiko
makubwa na mwenyekiti wa kamati ya sheria katika Bunge la Afrika
Mashariki ambaye pia ni mbunge kutoka nchini Kenya,Peter Mathuki
alipokuwa akielezea masikitiko yake kuhusiana na mawaziri hao kushindwa
kutikmiza wajibu wao.
Mathuki ameeleza kuwa tatizo lililopo
kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki la kutokuijua vema Jumuiya
hiyo ni kutofahamishwa mambo mengi yahusuyo Jumuiya na watu wenye wajibu
huo ni mawaziri husika.
Ameongeza kuwa kwa kipindi kirefu
sasa mawaziri hao hawajatokea wala kushiriki vikao vya Bunge hilo japo
wanatakiwa kufanya hivyo ili kuweza kufikisha ujumbe kwa wananchi ambao
ndio walengwa wakubwa katika kujua mambo mbalimbali ya nchi zao.
Mathuki
amedhamiria kuletamuswada katika Bunge hilo utakaoazimia kuwakataa na
kuwafukuza Bungeni hapo mawaziri wote hao ambao kwa mujibu wake anadai
wameonyesha utovu wa nidhamu kwenye Bunge hilo.
Katika
suala jingine, Mathuki amezungumzia umuhimu wa kutumia lugha ya
kiswahili katika vikao mbalimbali vya Bunge hilo ambapo pia imeonekana
ni sababu tosha kwa wananchi wengi kutojua mambo mengi ndani ya Jumuiya
kutokana na ugumu wa lugha ya kiingereza inayotumika na kongeza kuwa
inatakiwa kutumika sasa.
Amezitaka nchi zote kwa kutambua
na kukienzi kiswahili wanatakiwa kuhakikisha kinakuwa ni lugha ya kila
Taifa na itumike katika kufundishia mashuleni na hata katika matumizi ya
kila siku ya lugha hiyo.