Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kitengo kinachoshughulikia Tsunami, Ardito
Kodijat akifungua mafunzo hayo kwa kuwaeleza washiriki aina ya mafunzo
ambayo watapatiwa
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira
Rodrigues akitoa neno la ufunguzi kwa niaba ya UNESCO Tanzania na
kueleza sababu ya kufanyika mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kufanyika kwa siku tano.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja
Mkuu wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa
nchini (TMA, Dk. Ladislauds Chang`a akizungumza jinsi TMA imejipanga
kuendeleza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Tsunami na kuwataka
Watanzania kuwa na utaratibu wa kufatilia hali ya hewa nchini hasa
katika kipindi hiki ambacho ni kuna mabadiliko ya tabia ya nchi.
Watanzania wapata fursa ya kushiriki mafunzo kuhusu Tsunami
Kutokana
na kuwa na athari kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa,
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha
watu mbalimbali nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga.
Akizungumzia
Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira
Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata
elimu kuhusiana na Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo
yanasababishwa na hivyo ni matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa
kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine.
"Watu wengi
wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000
walipoteza maisha kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa
kiasi gani Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na
hapa," alisema Bi. Rodrigues.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema
kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa
yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo lilitokea eneo
lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na
kusababisha vifo vya waogeleaji watano.
"Mafunzo haya
yanatakiwa kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika
mengine na yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha
kufanya siku athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila
mtu kujua athari za Tsunami hata likitokea mbali," alisema Dk.
Chamuriho.