Naibu Spika wa Bunge atinga kwenye show ya Lady Jay Dee mjini Dodoma

Mwanamuziki Nyota wa Kike nchini Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee anayetamba na kibao chake cha #NdiNdiNdi amefanya onyesho alilolipa jina la #NaamkaTenaTour katika viwanja vya Royal Village, onyesho lililohudhuriwa na watu na watu mbalimbali akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Waheshimiwa Wabunge, Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez pamoja mashabiki wake mkoani Dodoma.
Na Zainul Mzige, Doodoma
Catherine Magige utambulisho
Mratibu wa show ya Lady Jay Dee ya Naamka Tena Tour ya mjini Dodoma, Mh. Catherine Magige akizungumza machache na kutambua uwepo wa Naibu Spika wa Bunge na waheshimiwa wabunge wenzake katika viwanja vya Royal Village mjini humo. (Picha zote na Zainul Mzige)
Bongo Flava Quee, Lady Jay Dee
Malkia wa Bongo Flava, Lady Jay Dee katika ubora wake.
Lady Jay Dee at Royal Village
Lady Jay Dee na The Band
Mwanamuziki Lady Jay Dee na The Band wakitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake katika harakati za kuwafikia mashabiki wake wote nchini nzima kwa show aliyoi' brand' kama Naamka Tena Tour.
Judith Wambura aka Lady Jay Dee
John Music
Mkali wa R & B kwenye Band ya Lady Jay Dee, John Music akitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma.
Lady Jay Dee - The BAND
Vijana watanashati wa bendi Lady Jay Dee wakitoa burudani kwa mashabiki wa Dodoma.
Mh. Kigwangalla
Hoyce Temu, Esther Bulaya, Shyrose Bhanji na Hamisi Kigwangalla wakipiga shwangwe kwa Lady Jay Dee alipokuwa jukwaani.
Mh. Shyrose Bhanji
Dk. Tulia Ackson na Alvaro Rodrihuez
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwenye viwanja vya Royal Village ilipofanyika show ya mwanamuziki Lady Jay Dee mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Alvaro Rodriguez at Lady Jay Dee concert
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mh. Shyrose Bhanji kwenye show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Esther Bulaya akiserebuka
Mh. Esther Bulaya akiserebuka na Hoyce Temu katika show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa juma mjini Dodoma.
Halima Mdee kwenye show ya Lady Jay Dee
Mh. Halima Mdee, Mh. Catherine Magige, Mh. Esther Bulaya pamoja na Hoyce Temu wakiserebuka.
Halima Mdee na Alvaro Rodriguez
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kawe, Mh. Halima Mdee walipokutana kwenye show ya Lady Jay Dee.
Lady Jay Dee akishambulia jukwaa
Mwanamuziki Lady Jay Dee na Band yake wakishambulia jukwaa.
Mashabiki wa Dodoma wa Lady Jay Dee
Mashabiki wa Lady Jay Dee wakiserebuka kwa raha zao.
Mashabiki wa Lady Jay Dee Dodoma
Pichani juu na chini ni Umati wa wakazi wa mjini Dodoma eneo la VIP wakiwemo waheshemiwa wabunge wakisakata muziki wa Lady Jay Dee.
Nyomi kwa Lady Jay Dee Dodoma
Patashika nguo kuchanika
Upendo waliounyesha watu wa Dodoma kwa mwanamuziki Lady Jay Dee.
Naamka Tena Concert Dodoma
Halima Mdee akipata Ukodak
Mh. Halima Mdee akipata Ukodak na wananchi wa Dodoma wanaomkubali.
Shyrose Bhanji na Hoyce Temu
Mh. Shyrose Bhanji na Hoyce Temu wakikumbatiana walipokutana kwenye show ya Lady Jay Dee mjini Dodoma.
Umati katika show ya Lady Jay Dee Dodoma
Mariam Nnauye wa Space Africa
Mh. Catherine Magige na Mariam Nnauye wakitoka jukwaani kumtunza Malkia wa Bongo Flava nchini, Lady Jay Dee.
Mh. Magige
Mh. Catherine Magige katika ubora wake.
Mariam Nnauye
Mheshimiwa Catherine Magige na Mariam Nnauye wakipozi kwa picha.
Binti Machozi, Lady Jay Dee
Lady Jay Dee akiwapa raha mashabiki wake na muziki wa Live.
Hamisi Kigwangalla
Waheshimiwa wabunge Hamisi Kigwangalla na Bonnah Kaluwa wakisakata burudani katika ukumbi wa Roya Village mjini Dodoma.
Mama Ankal Issa Michuzi
Mama Ankal Michuzi (mwenye nguo nyekundu) akijumuika na mashabiki wa Lady Jay Dee kuzungusha mduara.
Mama Ankal Michuzi
Didi Nafisa
Katika mkusanyiko huu kwa mbaaali anaonekana Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson akicheza kwaito eneo la VIP na mashabiki wa Lady Jay Dee.
Hoyce Temu kwaito
Kwaito likiendelea kunoga.
Catherine Magige
Mheshimiwa Catherine Magige ambaye ni rafiki na shabiki mkubwa wa Lady Jay Dee akicheza na kuimba kwa raha zake.
Mh. Catherine Magige
Beatrice Mkiramweni
Dada Beatrice Mkiramweni na Didi Nafisa wakijimwaga kwenye dancing floor.
Hoyce Temu
Mwanadada Hoyce Temu na mfanyakazi mwenzake Didi Nafisa wakionekana kuguswa na nyimbo za mwanamuziki Lady Jay Dee.
Bonnah Kaluwa katika Show ya Lady Jay Dee
Waheshimiwa wabunge akiwemo, Mh. Bonnah Kaluwa na Mh. Mboni Mhita pamoja wa wabunge wenzao nao walikuwepo kwenye show ya Lady Jay Dee.
Shyrose Bhanji, Esther Bulaya na Hoyce Temu
Kutoka kushoto ni Hoyce Temu, Mh. Shyrose Bhanji, Esther Bulaya pamoja na Didi Nafisa wa UN Tanzania.
Malkia wa Bongo Flava Tanzania, Lady Jay Dee
Lady Jay Dee katika ubora wake.
Lady Jay Dee akikonga nyoyo za mashabiki
Mwanamuziki Lady Jay Dee akikonga nyoyo za mashabiki wake akiwemo mmoja wa waheshimiwa wabunge ambaye alishindwa kuvumilia na kupanda jukwaani kucheza nae.
Lady Jay Dee Dodoma
Owen Mwandumbya
Beatrice Mkiramweni kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (kushoto) akisisitiza jambo kwa Afisa Habari wa Bunge, Bw. Owen Mwandumbya (katikati) wakati wa show la Lady Jay Dee ya 'NaamkaTenaTour' mjini Dodoma ambapo amepanga kuzunguka mikoa yote ya Tanzania. Kulia ni Mtalaamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post