Mwanamuziki wa R&B nchini Tanzania Rama D, amekanusha vikali habari
zilizotapakaa mtandaoni kwamba kwa sasa anatoka kimapenzi na
mwanadada Lady Jay Dee, amesema wanaheshimiana sana na haiwezi
kutokea kitu kama hicho daima .
Hata hvyo Rama D ameendelea kusema kwamba yeye anamfaham mpaka
mpenzi wa mwanadada Lady Jay Dee na kusema hata siku ya show ya
‘Naamka Tena Concert’ alipanda jukwaani kuonesha jinsi anavyomkubali
mwana dada huyo.
Rama D anasema anawashangaa sana watu wanaoenda kufanya video zao
nje na kusema kwamba haoni sababu ya kufanya video hizo nje kwani hapa
nyumbani kuna mazingira ya kutosha kufanya video nzuri zitakazoitangaza
nchi.