NA, MWANDISHI WETU
TANGA
MSANII wa Mziki wa
Bongo Fleva nchini Tanzania Navy Kenzo anatarajiwa kutumbuiza kwenye shindano
la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga Miss Tanga 2016 litakalofanyika Julai 29
mwaka huu kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach
Resort.
Licha ya Navy
Kenzo wasanii wengine ambao watasindikiza onyesho hilo kwa kutoa burudani ni
kundi la mziki wa kizazi kipya mkoani Tanga,Wazenji Classic pamoja na
Dances.
Akizungumza
jana,Mratibu wa Onyesho hilo, alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo
yanaendelea vizuri ambapo tayari warembo watakaoshiriki wameanza kuingia
kambini .
Shindano hilo
ambalo limeandaliwa na kituo cha Radio cha TK FM 88.5 kilichopo mjini Tanga kwa
kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wameelezea namna walivyo jipanga
kuhakikisha onyesho hilo linakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya
warembo waliopo .
“Nisema tu tumejiandaa
vizuri kuhakikisha
shindano hilo linafanyika kwa umakini mkubwa ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya
urembo mkoani hapa kuweza kupata ladha halisi ya onyesho hilo kwani licha ya
kuwaona warembo wakali wakini pia mzee wa kamatia chini atakuwepo kuwapagawisha
“Alisema.
Hata hivyo alisema
kuwa mazoezi ya warembo watanaoshiriki onyesho hilo yanaendelea kwenye ukumbi
wa New Hotel uliopo mjini hapa kuanzia saa kumi
jioni.
Aidha alisema kuwa
kabla ya kufanyika shindano hilo warembo hao watapata fursa ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani hapa ikiwemo Mapango ya Amboni
na Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha