MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA WALIA NA HUDUMA ZA AFYA

 wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Arusha  Ally Mtumwa akimkabidhi afisa ustawi wa jamii ambaye pia ni muangalizi wa mabusu ya watoto Mussa Mkamate magodoro ambayo jumuiya iyo waliwapelekea kama msaada hii leo
wa pili kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Arusha  Ally Mtumwa akifuatiwa na  mjumbe wa  Jumuiya ya wazazi  CCM wilaya ya
Arusha ambaye pia ni afisa masoko wa Radio Triple A Fm iliopo mkoani
Arusha Phidecia Mwakitalima wa pili kulia ni katibu wa wazazi CCM  wilaya Arusha Rehema Mohamed akifuatiwa na afisa ustawi wa jamii wa mahabusu ya watoto Arusha
Na Woinde Shizza ,Arusha

Mahabusu ya watoto  jijini Arusha inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ukosefu wa huduma za kiafya ikiwemo madawa  pamoja na muhudumu
wa afya anaehudumia watoto waliopo katika mahabusu hiyo.

Ayo yamebainishwa jana  na Afisa ustawi wa jamii ambaye pia ni
misimamizi wa mahabusu ya watoto Mussa Mkamate  wakati alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa
magodoro 25 kutoka kwa jumuiya ya wazazi wa CCM wialaya ya Arusha .

Alisema kuwa mahabusu hiyo ya watoto imekuwa ikisumbuliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ukuta wa mahabusu ,ukosefu wa
 walinzi wa mahabusu hao ambao ni watoto hali ambayo inasababisha
wakati mungine watoto hao kuweza kutoroka katika mahabudu hiyo.

Mbali na hayo pia afisa ustawi wa jamii hiyo aliitaka serekali kuweza
kusaidia mahabusu hiyo kuwa na vitendea kazi ikiwemo usafiri wa watoto
wao pindi wakiwa wanaumwa gafla pamoja na pale wanapopelekwa
mahakamani kwani alibainisha kuwa muda mungine iwapo mahabusu motto
anapoumwa viongozi ambao waliopo katika mahabusu hiyo wanalazimika
kutoa fedha mifukono kwao na kukodisha usafiri kwa ajili ya kumpeleka
mtoto huyo hospitalini.

“pia kumekuwa na tatizo kubwa la ucheleweshaji wakusikiliza kesi za
hawa watoto unakuta mtoto amekaa mahabusu kwa muda mrefu na kesi yake
aisikiliswi pia napenda sana kuiomba serekali itusaidie kuarakisha
kesi hizi za hawa watoto ili ziweze kusikilizwa kwa haraka na kwa
wakati “alisema Mussa
Aliongeza kuwa pia wamekuwa wanakutana na changamoto ya kutokuwepo kwa
mahakimu wa kusikiliza kesi za watoto hali ambayo inalazimu kesi hizi
za watoto kusikilizwa katika mahakama ya mwanzo ambapo muda mungine
mahakimu waliopo katika mahakama hizi za mwanzo wamekuwa wakitoa
hukumu pasipo kumuangalia umri wa mtoto.

“kama ivi kati kuna mtoto kashtakiwa kakubali kosa baada ya kukubali
kosa kahukumiwa miaka miwili na mtoto huyo anaumri wa miaka 12  mbali
na ivyo ikirudi kwenye katiba au sheria ya nchi hairuhusu mtoto
kuhukumiwa kifungo anatakiwa kupewa adhabu sasa hii inaumiza sana sasa
tunaomba serekali angalau ianzishe mahakama ya watoto ili kuweza
kutatua tatizo hili kwani bila kufanya hivyo itapelekea kuendelea
kuwaumiza watoto wetu hawa ata kama wanamakosa”alisema Musa.

Kwa upande wake mjumbe mmoja wa Jumuiya ya wazazi  CCM wilaya ya
Arusha ambaye pia ni afisa masoko wa Radio Triple A Fm iliopo mkoani
Arusha Phidecia Mwakitalima aliiomba serekali kuweza kusadia kuongeza
maafisa ustawi wa jamii ambao wataenda na watoto hao mahakamani
kuwasikilizia kesi zao na kubainisha kuwa iwapo maafisa ustawi
watakuwa wengi basi inaweza kusaidia pia hata hawa watoto kupata
hakizao za kimsingi wanapopelekwa mahakamana na hata pale wanapokuwa
mahabusu.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post