UNESCO YAWAFUA WATENDAJI WA REDIO JAMII
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio
Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiwakaribisha na
kuwatambulisha wawezeshaji kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
siku tano ya kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na Tehama kwa
mameneja na waandishi wa habari takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali
nchini, yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio
Sengerema mkoani Mwanza.
Na
Mwandishi wetu, Sengerema
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) limesema litaendelea kusaidia kuimarika kwa redio za
jamii nchini kwa kuwa ndio nyenzo muhimu za maendeleo ya wananchi kwa
kuwapa sauti katika huduma na shughuli zao.
Kauli
hiyo imetolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO,
Bw. Al Amin Yusuph, wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa mameneja na watendaji
takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, mafunzo yanayofanyika
kwenye kituo cha Redio Sengerema FM.
Katika
mafunzo hayo watendaji hao watafunzwa masuala ya Tehama na utafutaji wa
soko kwa lengo la kufanya redio hizo kuwa endelevu na kujiendesha zenyewe
kwa kuweza kutekeleza miradi yake na kuendelea kushirikiana na
wananchi.
Mafunzo hayo ni utekelezaji wa mradi wa miaka mitatu wa
kuwezesha redio za jamii nchini unaoendeshwa na UNESCO baada ya redio hizo
nyingi kusaidiwa kuanzishwa katika miaka ya karibuni.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akizungumza na Mameneja na waandishi wa habari
kutoka redio tisa za jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya kuwajengea
uwezo katika masuala ya masoko na matumizi ya Tehama yanayofadhiliwa na
mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu
Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Kushoto mgeni rasmi Ofisa mdhani kutoka
Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya
usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed.
Kwa
mujbu wa Yusuph mradi wa SIDA ambao umekuwa ukitekelezwa kwa kipindi cha
miaka mitatu umeshughulika na uboreshaji wa redio hizo ili kuzipatia
uwiano na pia kuziwezesha kutumia Tehama kuhabarisha wananchi pia kutokana
na mafanikio yaliyopatikana mradi huo utaendelea kwa miaka mingine
mitatu.
Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana kwa ushirikiano
wa Redio za jamii pamoja na shirika hilo hali iliyofanya kuyavuta mataifa
mengine kuchangia kwa ajili ya kuendelea kuzijengea uwezo redio za jamii
kupitia shirika hilo.
Ameongeza kuwa kufanikiwa kwa redio za jamii nchini
Tanzania katika mradi huu wa SIDA kumefanya mashirika mengi yanayotaka
kufanyakazi na wananchi wa kawaida kukimbilia UNESCO kutambua redio za
jamii ambazo zinaweza kufanyakazi nayo.
Mradi
huo wa Tehama unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na
kuratibiwa na UNESCO ni sehemu ya mradi wa UNESCO katika nchi saba za
Afrika , Tanzania ikiwamo.
Baadhi ya Mameneja na waandishi wa habari kutoka
redio mbalimbali za jamii wakimsikiliza Bw. Al Amin Yusuph kwenye ufunguzi
wa mafunzo hayo yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano
Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
Katika
mafunzo hayo yanayofanyika mjini Sengerema, elimu inatolewa kwa wakuu wa
vituo na waandishi wa habari kutoka redio Micheweni FM, Orkonerei FM,
Pambazuko FM, Mtegani FM, Kahama FM, Redio FM, Kyela FM, Fadeco Radio na
Pangani FM.
"Kuna
mambo mengi yamefanikiwa.. kikubwa zaidi kumpa nafasi mwananchi kujieleza
na kueleza matumaini yake.." alisema Yusuph ambapo aliongeza kwamba
kutokana na mradi huo kufanikiwa zipo nchi na mashirika ambayo yapo tayari
kuchangia uimarishaji wa redio za jamii nchini.Hakuzitaja nchi
hizo
Alisema kutokana na mafanikio yaliyopo ya redio hizo
kuwa karibu na jamii, SIDA kwa kushirikiana na UNESCO wametengeneza
programu hiyo ili kuwezesha kuwepo kwa matumizi ya mtandao katika kukusanya
habari, kuziboresha na kuzitumia kwa manufaa ya
wananchi.
Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni
Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii
Micheweni, Ali Mohamed, akitoa baraka zake tayari kuanza mafunzo ya siku
tano ya kuwajengea
uwezo katika masuala ya masoko na Tehama mameneja na waandishi wa habari
takribani 60 kutoka redio za jamii mbalimbali nchini, yanayoendelea kwenye
kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani
Mwanza.
Alisema kutekelezwa kwa mradi huo ni utekelezaji wa
azimio la Windhoek la mwaka 1991 linalohimiza matumizi ya redio jamii
katika kuboresha maisha ya wananchi kutokana na kuonekana dhahiri kwamba
wananchi wanapokuwa na nafasi ya kujieleza wanaweza kufanya makubwa
zaidi.
Akifungua mafunzo hayo Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya
Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi
redio jamii Micheweni, Ali Mohamed aliwataka mameneja na watendaji wa
radio hizo kutekeleza ushauri wa UNESCO ikiwa na pamoja na kutekeleza
maagizo ya utengenezaji wa vipindi vya vijana ili kupata nafasi ya
kushindania nafasi moja ya upendeleo kwenda Paris , Ufaransa mwakani kwa
tamasha la redio za jamii.
Aidha
aliwataka watendaji kuwa makini katika kazi zao kutokana na serikali kuweka
mazingira sahihi ya uendeshaji wa radio hizo kwa manufaa ya
umma.
Mkufunzi wa darasa la mameneja wa redio mbalimbali za
jamii Mkurugenzi Mtendaji wa ASMET, Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo
ya siku tano ya namna ya kuingiza kipato pamoja na kutafuta masoko kwa
ajili ya kuendeleza vituo vyao yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na
kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema
Telecentre mkoani Mwanza.
Baadhi ya mameneja wa redio mbalimbali za jamii
wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya masoko na ujasiriamali
yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Meneja wa kituo cha redio Orkonerei FM, Bw. Lucas
Kariongi akihoji swali kwa mkufunzi wakati wa mafunzo
hayo.
Mhasibu wa kituo cha habari na mawasiliano Sengerema
Telecentre, Bw. George Tumbo akiongaza washiriki wenzake katika kazi za
vikundi wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akiendesha mafunzo ya matumizi ya Tehama
kuwajengea uwezo wa kuweka kumbukumbu za vipindi na kukusanya vyanzo vya
habari kwa kutumia "Tablet" kwa waandishi wa habari wa redio mbalimbali za
jamii yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na
kuratibiwa na shirika la UNESCO yanayoendelea kwenye kituo cha Redio
Sengerema mkoani Mwanza.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akitoa maelekezo ya matumizi ya "TABLET" katika kuhifadhi na kuandaa habari
kwa kutumia kifaa hicho.
Pichani juu na chini ni washiriki wa mafunzo
hayo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya
"TABLET".
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia