WATANZANIA WATAKIWA KUONA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA(NIC) NI MALI YA UMMA

Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani
Arusha Nyerembe Munasa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya
kutembelea banda la Shirika la Bima la Taifa (NIC) katika maadhimisho ya
wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa jijini
Arushaa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid, ,aliyeshika mice ni meneja wa shirika hilo Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin Ole Kambaine
Meneja
wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin
Ole Kambaine akitoa maelezo mafupi kuhusu shirika hilo kwa Mkuu wa
wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa mara baada ya kutembelea
banda hilo jijini Arusha katikati ni meneja masoko na utafiti wa
shirika hilo kutoka makao makuu Bw.Elisante Maleko
Mdau aliyetembelea banda hilo la
Shirika la Bima la Taifa (NIC) akiwa anauliza maswali yanayohusu
shirikika hilo lengo nikutaka kufahamu zaidi shughuli za shirika,kushoto
ni Afisa wa Bima Bi.Costancia Komanya

Meneja masoko na utafiti wa
shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoka makao makuu Bw.Elisante Maleko
akiwa anatoa ufafanuzi kwa mdau aliyefika katika banda lao ambapo
alisema kuwa pamoja na bima nyingine pia wanatoa huduma ya bima ya
matibabu (madecare) ambao ni mpango maalum wa shirika hilo kutoa
matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kaumwa na michango ni
midogo

Muonekano wa banda la shirika la Bima la Taifa (NIC) katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabaranijijini Arusha
Meneja masoko na utafiti wa shirika
la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elisante Maleko amewataka watanzania kuona
shirika hilo ni mali yao kwa kuwa shirika hilo ni mali ya umma na
michango ni midogo hivyo kila mwananchi kumudu
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na
wadau mbalimbali waliyotembelea banda lao katika maadhimisho ya wiki ya
nenda kwa usalama barabarani yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid jijini Arusha
Bw.Maleko alisema kuwa shirika hilo lina
bima ya matibabu amabayo ni mpango maalum wa shirika hilo kutoa kinga ya
matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kuumwa na michango ni
midogo na kila mwananchi anamudu kujiunga na huduma zinapatikana nchi
nzima
Pia alisema Bima za nyumba inakinga na
majanga ya wizi,moto,tetemeko na mafuriko hivyo kuwataka wananchi
kukatia nyumba zao bima
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia