ZAIDI ya bilioni 6 zimetumika kuwalipia wakina mama wajawazito na watoto katika vituo mbalimbali vya afya katika mikoa ya Tanga na Mbeya ambao ni wanachama na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kupitia mradi wa
(KFW).
Mradi huo unaendeshwa kwa
ushirikiano kati ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Benki ya
Maendeleo ya watu wa Ujerumani (KFW) ambao unatekelezwa hapa nchini
katika mikoa ya Tanga na Mbeya.
Hayo yalibainishwa kwenye
ufunguzi wa mafunzo ya watoa huduma wa mradi wa (KFW) juzi na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Daudi Bunyinyiga
ambapo alisema kwa kiasi
kikubwa mradi huo umevuka
lengo la walengwa waliokusudiwa awali kuandikishwa katika mfuko wa Afya
ya Jamii(CHF) kupitia mradi huo.
Alisema kuwa wakati mradi huo
ulipoanzishwa ulitarajiwa kuwahudumia akina mama wajawazito 80, 0000
katika kipindi cha miaka mitatu ya mradi huo wakati mpaka sasa
umeandikisha na kuwahudumia akina mama
wajawazito 190,631 kwa mikoa ya Tanga na Mbeya hivyo kuvuka lengo kwa asilimia 238.
Bunyinyiga ambaya pia ni Meneja wa Miradi inayosaidiwa na wahisani alisema kuwa kwa mkoa wa Tanga fedha zilizotumika zilizokuwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 958 ambapo mradi huo umeweza pia kutumia
kiasi cha shilingi milioni 989.1 kwa ajili ya kununulia vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kujifungulia, mashine za kutakasia vifaa zilizovyokwisha kugawiwa kwa mikoa ya Tanga na Mbeya.
Akizungumzia kuhusu mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF) alisema kuwa Jumla ya Shilingi bilioni 1.5 zimelipwa
katika Halmashauri mbalimbali ili kuwaandikisha akina mama hao na
familia zao katika mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF).
Alisema kuwa lengo la
kuwaandikisha akina mama hao na familia kwenye (CHF) ni kuhakikisha
wanapata huduma endelevu baada ya kumalizika kwa muda wa kupata huduma
katika mfuko wa Bima ya Afya ambapo huduma hizo ni kwa kipindi cha mwaka
mmoja.
Awali akizungumza wakati wa
ufunguzi huo, Katibu Tawala wilaya ya Korogwe Stanley Lameck ambaye
alimuwakilisha Katibu tawala mkoa wa Tanga,Salum Chima alisema kuwa
mpango huo wa KWF kwa mkoa umekuwa na mafanikio makubwa hasa ukizingatia
kuwa kundi la walengwa wa awali wanawake na wototo ndio waliokuwa na
changamoto kubwa ya huduma za matibabu tangu hatua za mwanzo za ujauzito
hadi kujifungua.
Alisema kuwa kupitia mradi huo
idadi ya wanawake wanaojifungulia katika vituo vyakutolea huduma
imeongezeka kutoka asilimia 48 mwaka 2011 hadi zaidi ya asilimia 60
mwaka 2013.
Hata hiyo alisema kuwa vifo
vya wakina mama vinayotokana na matatizo ya uzazi wakati wa kujifungua
vimepungua kutoka 110 mwaka 2013 hadi kufikia 69 kwa mwaka 2014 ikiwemo
kwa watoto wachanga chini a mwezi mmoja kutoka 275 kwa mwaka 2013 hadi
kufikia 206 mwaka 2014.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia