Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Tuhuma za rushwa na uporaji wa mali za Manispaa ya
Moshi, mkoani Kilimanjaro, zimesababisha vurugu zilizopelekea kikao cha
Baraza la Madiwani kumkataa Mkurugenzi, Shaaban Ntarambe, huku
likipitisha azimio la kumburuza mahakamani kwa ubadhirifu.
Meya wa Manispaa hiyo, Jaffary Michael, akizungumza mara baada ya
kuvunjika kwa Kikao cha Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Manispaa hiyo
kwa mwaka 2015/2016, alisema madiwani hao wamepanga kumwandikia barua
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (pichani), wakimtaarifu kuhusu hatua
watakazochukua dhidi ya Mkurugenzi huyo, ikiwamo kufungua mashtaka
mahakamani.
“Tumetenga zaidi ya Sh. milioni 124 kwa ajili ya kufanya usajili wa
viwanja vyetu, lakini fedha hiyo hiyo imeanza kutuletea balaa,
Madiwani wangu wamejiridhisha, nami ni shahidi,” alisema.
Alisema Mkurugenzi amehusika baada ya kuondoa kwa siri, zuio la
Baraza kwa Msajili wa Hati na kutengeneza hati kwa ajili ya kuwapatia
matajiri wachache waliojificha nyuma ya kikundi, kinachojiita Mawenzi
Sports Club, akishirikiana na watendaji …viwanja vyote vya umma
vilivyobaki havina hati haviko salama tena,” alisema Meya.
Kabla ya kuvunjika kwa kikao hicho, ambacho kilihudhuriwa pia na
Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi (Das), Remida Ibrahim, aliyemwakilisha
Mkuu wa Wilaya; Diwani wa Kata ya Rau (Chadema), Peter Kimaro, baada ya
sala alimshambulia Ntarambe, akidai amehusika katika uporaji wa uwanja
wa Mawenzi wenye hati namba 10660 (056035/12).
Baada ya hoja hiyo, madiwani 24 kati ya 29 wanaounda Baraza hilo,
walitoka nje wakitaka Mkurugenzi huyo awajibike kwa kujiuzulu wadhifa
wake au aondoke Moshi kabla ya kumburuza mahakamani.
Mgogoro huo ulilipuka zaidi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Mipango Miji, Ardhi na Mazingira, Rey Mboya, kudai eneo hilo limeporwa
kutokana na nguvu ya watendaji kuamua kutengeneza hati nyingine
kinyemela.
Wakati vurugu hizo zikitokea, madiwani wanne wa CCM, Apaikunda
Naburi (Mawenzi), Priscus Tarimo (Kilimanjaro), Miriam Kaaya (Viti
maalum) na Michael Mwita (Kaloleni), walijibizana kwa maneno makali na
Meya kwa madai ameshindwa kutenda haki kwa kumruhusu Tarimo kuuliza
swali kabla ya kuanza kwa kikao.
Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo, alisema licha
ya Halmashauri hiyo kuongozwa na Chadema, hawawezi kuungana na kukubali
watendaji wachache na baadhi ya wanasiasa kuiba mali za umma.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Halmashauri hiyo, Mkurugenzi wa Mipango
Miji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mwaka
2001 aliidhinisha eneo hilo ni mali ya umma baada ya kupigwa kwa picha
za anga kati ya mwaka 1998 na 1999.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia