BREAKING NEWS

Thursday, January 15, 2015

SOMA JINSI WAGOMBEA WA URAIS SITA WALIVYOKOMALIWA NA CCM

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM , mjini Unguja , Zanzibar.Kushoto ni Makamu wake (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein
 Wakati Kamati Kuu ya CCM, ikieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya viongozi wake walio katika dhamana ya kisiasa kukumbwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow, adhabu kali zitachukuliwa dhidi ya wagombea urais sita walioadhibiwa mwaka jana endapo walikiuka masharti ya adhabu zao.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jana baada ya Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana Ofisi Ndogo ya CCM, Kisiwandui kuwa kamati hiyo imeagiza Kamati Ndogo ya Maadili kushauri na kuwachukulia hatua za kinidhamu viongozi watakaokuwa wamekiuka adhabu husika.
“Itakumbukwa kuwa kuna makada sita wa CCM waliopewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao Februari mwaka huu.
“Baada ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia masharti ya adhabu zao na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao, wataongezewa adhabu,” alisema Nape.
Vigogo sita waliopewa adhabu ni; Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira .
Wengine ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Nape alisema kamati ndogo ya maadili inayoongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula itatoa ushauri kwa ngazi za juu za CCM na ikibidi hatua nyingine za kinidhamu na kiatiba zitafuata.
Makamba asema
“Binafsi sina wasiwasi, kwanza mwanzoni sikustahili kuwemo na hata sasa sina shaka kama kuna lolote nililofanya kinyume.”
Alisema kuwa wanaopaswa kuwa na wasiwasi ni wale wanaogawa pesa. “Sisi wengine hizo fedha hatuna...ninaamini wapo wengine ambao hawapo kwenye orodha lakini wamekiuka maadili. Nilitarajia na wao watahojiwa,” alisema Makamba.
Sumaye akumbushia rufani
Akizungumzia hatua hiyo ya Kamati Kuu, Sumaye alisema: “Mimi siwezi kujitathmini mwenyewe, tusubiri hiyo kamati tuone, sijui watasema nini na wala sielewi kosa langu na ndfiyo maana nilikata rufani.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates