Katika
picha kulia Mwenyekiti mpya wa mtaa wa kaloleni jijini Arusha Abdul
Nassor juzi alikabidhi matofali 100 kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi
kaloleni mama Raymond Pudensian kwaajili ya ujenzi wa uzio wa shule hiyo inayokabiliwa na changamoto ya uzio
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kaloleni mama Raymond Pudensian akisoma taarifa ya shule kwa uongozi wa mtaa wa kaloleni baada ya mwenyekiti Abdul Nassor kukabidhi matofali 100 kwaajili ya ujenzi wa uzio wa shuleKatibu wa CCM wilaya ya Arusha, Feruz Bano akizungumza ambapo alisisitiza watu kujitolea kama alivtofanya mwenyekiti wa mtaa huo
Wanafunzi wakiwa wanasukuma mashine kwaajili ya kutengeneza kisima cha maji
Mwanafunzi mwenye tatizo la utindio wa ubongo akiwa anaosha vyombo shuleni hapo
Hapa baadhi ya wanafunzi wenye tatizo la utindio wa ubongo wakiwa darasani
Picha ya pamoja
Wanafunzi wakiwa katika darasa la vitendo
Shule
ya msingi ya kaloleni na makumbusho iliyopo katika halmashauri ya jiji
la Arusha inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio
shuleni hapo hali inayochangia utoro kwa wanafunzi
Kutokana na changamoto hiyo mwenyekiti
mpya wa mtaa wa kaloleni Abdul Nassor jana alikabidhi matofali 100 kwa
mwalimu mkuu wa shule ya kaloleni kwa ajili ya ujenzi wa uzio
utakaotumika pia kwa shule ya msingi ya makumbusho
Mwenyekiti
Nassor alisema aliguswa kuchangia mchango huo kutokana na hali halisi
ya shule hiyo kukosa uzio hali ambayo pia kiusalama kwa wanafunzi
wanaosoma hapo kuwa mdogo
Aliwataka wadau mbalimbali na hata waliowahi kusoma katika shule hizo kujitokeza kuchangia katika ujenzi wa uzio wa shule
Kwa
upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kaloleni mama Raymond
Pudensian akipokea msaada huo alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya uzio
shuleni hapo hivyo aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia
matofali kwaajili ya ujenzi huo.
Bi
Pudensiana alitaja makadirio ya matofali 5000 yanahitajika kwaajili ya
uzio wa shule hiyo na kwa kukamilika kwa uzio huo itasaidia mauzurio
mazuri kwa wanafunzi pamoja na usalama wa kutosha
‘’Kutokana
na shule yetu kupakana na mto kwakweli hali ya kiusalama ni mdogo kwa
kuwa hata wanafunzi wanaweza kwenda kujificha huko ila uzio ukikamilika
itakuwa imesaidia kwa kiwango kikubwa”alisema Pudensiana