BREAKING NEWS

Monday, January 19, 2015

JAMII YASHAURIWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU KWA JESHI LA POLISI


 Na Mahmoud Ahmad Dar es Salaam   
JAMII imeshauriwa kuendelea kutoa taarifa kwa jeshi la polisi dhidi ya watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kwani wasababisha uvunjifu wa amani kwa raia na mali zao.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi.Sophia Mjema,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya utoaji sifa na zawadi kwa maofisa wakaguzi na askari 107 wa vyeo mbalimbali,kutokana na umahili wao wa kupambana na uhalifu kwa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam.

Bi.mjema alisema kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na kuwakamata wahalifu ambao ndio chanzo cha uvufu wa amani,hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana na poli kwa ajili ya usalama wao na  taifa kwa ujumla.

Aidha aliwataka wale wanaomiliki silaha kihalali wazitumie kwa kufuata sheria na si vinginevyo,pia waache tabia ya kuwatishia raia wenzao kwa kuwa wanaumiliki halali,na endapo watabainika na tabia hizo watanyang’anywa silaha zao mara moja.

“wapo baadhi ya watu huko mitaani wanamiliki silaha kinyume na taratibu za kisheria,msiwafumbie macho wala kuwaonea muhali,hata kama ni ndugu yako tunaomba mtoe taarifa kwa jeshila polisi litawashughulikia,pia kuna baadhi ya wale waomiliki kihalali silaha hizo lakini wanazitumia kinyume cha sheria kwa kufanya uporaji na kuwatishia raia mitaani,suala ambalo ni la hatari na haliwezi kuvumiliwa likiendelea,hivyo hakuna budi kuwafichua ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi yao”

Bi.Mjema amewataka wajisalimishe haraka wale wote wanaomiliki silaha pasipo kufuata sheria,kabla jeshi la polisi halijaanza msako mkali,kwani atakayekutwa na silaha atafikishwa mbele ya dola kujibu mashtaka ya kukadi na kusababisha uvunjifu wa sheria.

Kwa upande wake Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Suleiman Kova,ameliomba jeshi la polisi kufanya kazi kwa weledi mpana zaidi,kwa kufuata misingi na taratibu zilizowekwa,katika kulinda na kufichua wahalifu,ili nchi iendelee kuwa na amani ambayo ndio tunu a taifa letu.

“Tunataka nchi hii iendelee kuwa kisiwa cha amani na hatukubali kabisa mtu yeyote alete chokochoko za aina yeyote awe chanzo cha kutoweka kwa amani yetu ambayo ni zawadi kutoka kwa mwenyezi mungu,kupitia waasisi wa yaifa hili ambao walituletea uhuru,hivyo nyinyi kama askari mhakikishe mnawakamata na kuwatia hatiani wale wote watakaothubutu kuhatrisha amani ya nchi”.alisema Bi. Njema

Naye  Mwenyekiti Wa Kamati Ya Ulinzi Na Usalama ambaye pia ni sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Musa Salum,alizungumzia suala la baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakijipitisha katika nyumba za ibada kufanya kampeni kwa manufaa yao binafsi ili wananchi wawape kura,kamwe suala hilo halikubaliki na wanatakiwa kujiheshimu na kuacha tabia hiyo mara moja.

“Tayari tumejipanga kikamilifu kuhakikisha wanasiasa wanaheshimu nyumba za ibada,na kwamba siasa zao wazifanyie uraiani na sio misikitini wala makanisani,na wananchi wawakatae viongozi wanaotumia pesa kuomba kura na wasiwachague”.

Aidha ametoa wito kwa tume ya taifa ya uchaguzi (nec),ifanye kazi yake kwa uadilifu na kwa makini zaidi kwa kuweka utaratibu ambao ni mzuri kwa wapiga kura katika chaguzi zijazo za katiba na uchaguzi mkuu ujao,na kuachana na mambo ya ubabaishaji ambayo yamekuwa yakileta taflani.
 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates