Balozi wa Heshima wa Taasisi ya
Kimataifa ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania (CILT), Waziri wa Jumuia
ya Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia), akizungumza katika
mkutano wa maandalizi ya kukusanya fedha kwa ajili ya mkutano wa
kimataifa utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 4 hadi 5
ulioandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajengea weredi wadau wa
usafirishaji kutoka nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi kutoka Cilt, Zacharia Hans Poppe.
Mwenyekiti wa CILT, George Makuke
(kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa
Mipango wa MOT, Migire Gabriel, Balozi
wa Heshima wa Taasisi ya Kimataifa ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania
(CILT), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe
na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Cilt, Zacharia Hans Poppe.
Mkurugenzi wa Mipango wa MOT, Migire Gabriel, akizungumza katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
IMEELEZWA kuwa ukosefu wa weledi na
utaalam wa masuala mbalimbali ya usafirishaji ndio chanzo cha kutokea
kwa ajili nyingi nchini.
Hayo aliyasema jana Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa Usafirishaji na Uchukuzi
nchini(FCILT), George Makuke wataki wakizungumzia maandalizi ya mkutano
mkubwa unaotarajiwa kufanyika Machi mwaka huu Mkoani Arusha.
Mkutano huo utahusisha nchi mbalimbali Duniani ukiwa na lengo la kujenga weledi katika masuala ya usafirishaji na uchukuzi.
Akizungumzia mkutano huo alisema kuna
mambo mengi yanafanyika katika usafirishai ambayo si sahihi hivyo
mkutano huo utasaidia wahusika kutoa huduma kihalali.
"Ukiangalia kumekuwa na udanganyifu
mkubwa katika masuala ya usafirishai kwa kuzidisha bei lakini hata watoa
huduma wenyewe wamekuwa hawana weledi hivyo mkutano huo utajadili namna
ya kuondia changamoto zote hizi"alisema
Kwa Upande wa Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe alisema kuwa mkutano huo ni
mkubwa hivyo atahamasisha taasisi mbalimbali kutoa michango yao kwani
unahitaji fedha nyingi kwaajili ya kuwahudumia wageni.
"Hasa nitaangalia namna gani taasisi za
Wizara ya Maliasili na Utalii wamechangia kiasi gani maana wao ndio
watakaofaidika kwani watu watatoka nchi mbalimbali hivyo itasaidia
kuitangaza nchi"alisema
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
ya Mkutano huo,Zakaria Hans pope, alisema mkutano huo utasaidia kukuza
uchumi kwani kama kukiwepo njia sahihi za usafirishaji mapato lazima
yaongezeke.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia