Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisaini Kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili Kwenye Ofisi ya Mtendaji kata ya Mlimani Katika
Mfululizo wa Ziara zake katika Kata mbalimbali Jimbo la Morogoro mjini.
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Vifuko vya mndihira
na Mwere Vilivyo Kata ya mlimani Ambavyo Vimegarimu Kiasi cha Shilingi
Milion 3 Zilizotolewa na Mbunge Huyo.
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akianda Safu ya Milima Uluguru
Kuelekea Mitaa ya Kisosa ,Choma na Chalagule vilivyopo Kata ya Mlimani
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza kwa Makini Kero
Mbalimbali zilizokuwa Zikiwasilishwa na wakazi wa Kata ya Mlimani Jimbo
la Morogoro Mjini wakati Mbunge huyo aliopofanya ziara ya Kutembelea
kata Hiyo.
Baadhi ya Wakazi wa Mitaa ya Ruvuma
,Mng'ong'o, na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani Wakimsikiliza kwa Makini
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini alipofanya ziara katika Mitaa hiyo ili
kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisisitiza Jambo wakati Akiongea na wakazi wa Kata ya Mlimani
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Mara
baada ya Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata ya Mlimani
Ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na
Barabara.Kuhusu Maji Mh Abood
alitoa Zaidi ya Shilingi Shilingi Milioni 20 Kwajili ya Kununua Vifaa
vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika Mitaa ya Kisosa ,Choma , Chalagule Ruvuma Mng'ong'o na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani. .Pia
Alitoa vifaa vyenye Dhamani ya Shilingi Milion 2 kwajili ya Kununua
Vifaa vya Kukarabati Barabara Za Mitaa hiyo Ikiwemo Sajuri,Makaravati
na Vifaa vingine vinavyotumika kutengeneza Barabara.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea zawadi Kutoka kwa Wakazi wa Mitaa ya Kisosa
,Choma na Chalagule Ikiwa ni Ishara ya kukubali Utendaji wa Kazi wa
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini.Wakielezea Zaidi wakazi hao wamesema
Tangu Uhuru hakuna Mbunge aliyewahi kuwatembelea na pili Ahadi zote
alizowahidi wakati wa Mitaa hiyo amezitekeleza na bado wana imani kubwa
sana na Mbunge Huyo.Namnukuu Mkazi Mmoja aliyejitambuliza kwa Jina la Bw
Omari Alisema " Huyu Ndiye Mbunge tunayemuhitaji Mbunge wa Vitendo na
si Mbunge wa Maneno Mengi Utendaji Hafifu"
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa na mtendaji wa kata ya
Mlimani mara baada ya kuwasili katika Mitaa ya Ruvuma Mng'ong'o na Tulo
Iliyopo Kata ya Mlimani.