WANANCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) WANAIPENDA MUUNGANO KULIKO VIONGOZI WAO



Itachukua muda mrefu kuwaamini wanasiasa katika nchi zinazoendelea, kwani mambo mengi wanayofanya machoni mwa watu sio ambayo yapo mioyoni mwao.
Utamuona kiongozi wa siasa anasaidiana na wananchi wake kulima na kufanya kazi nyingine kwa mbwembwe nyingi. Mwingine anahudhuria ibada kanisani au msikitini kwa unyenyekevu mkubwa.
Lakini wote hawa dhamira zao ni tofauti kabisa na mambo wanayotenda na hata kwa kuwatazama sura zao tu, utatilia shaka jambo wanalofanya.


Hivyo, kumuamini mwanasiasa kwa walau asilimia 70 tu, kunahitaji ufanye uchunguzi mkubwa juu ya nia yake.
Hili ndio lipo katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Wanasiasa wana dhamira tofauti na wananchi walio wengi.
Hivyo, hata pale, yanapoibuka majadiliano kwenye mambo ya msingi ya kisera au kimkataba, wanasiasa ndio wamekuwa vikwazo kwa nia njema au mbaya.
Utawasikia, wanasema wananchi hawataki jambo hili, wanataka hili, wanaomba tusubiri kwanza na wengine wana hofu na jambo fulani.

Haya yamekuwa majibu ya jumla ya wanasiasa pale wanapoona ajenda zao binafsi zinakwama au zipo hatarini.
Kufufuka kwa jumuiya






Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ambayo ilivunjika mwaka 1977, ililifuliwa tena Novemba 30, 1999. Ilipofika Julai 2000, makubaliano yalianza kutekelezwa.
Mchakato wa kufufua jumuiya hii, ulianza Novemba 1993 jijini Arusha, baada ya kikao cha marais wakati huo, Ali Hassan Mwinyi (Tanzania) Yoweri Museveni (Uganda) na Daniel Arap Moi (Kenya).
Baadaye mwaka 1996, Sekretarieti iliundwa na kuwezesha kuanza mazungumzo mapya ya kurejesha jumuiya hii na kwa mafanikio makubwa ndipo mwaka 1999 mkataba ukasainiwa.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post