arista Charles Makoi enzi za uhai wake.
MAZISHI ya Carista Charles Makoi, 52, (pichani), ambaye alikuwa mke wa mfanyabiashara bilionea jijini hapa, Charles Makoi yamefanyika huku shilingi milioni 200 zikisemekana kuteketea kwa bajeti.
Mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Patrick Ngiloi ambaye ni mmiliki wa vituo vya mafuta vya Kampuni ya Panone ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mazishi hayo.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali iliyosababisha kifo cha Carista Charles Makoi.Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya kamati hiyo, siku ya kwanza tu baada ya kifo hicho, saa tatu mbele zilichangwa zaidi ya shilingi milioni 75 na baada ya hapo ziliendelea kuchangwa hadi kufikia lengo.
Chanzo kilisema kuwa, wachangaji wakubwa walikuwa wafanyabiashara wakubwa kutoka mikoa ya kaskazini mwa Tanzania, ikiwemo Arusha, Kilimanjaro na Tanga.“Wengi waliowahi kuchanga ni wafanyabiashara wa mikoa hiyo niliyokutajia. Lakini tulidhamiria bajeti iwe ya milioni mia mbili. Unajua shughuli ni shughuli siku zote.