BREAKING NEWS

Saturday, January 24, 2015

HATIMAYE PROF MUHONGO ATANGAZA RASMI KUJIUZULU UWAZIRI WA NISHATI NA MADINI

 Prof Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari hii leo wakati akitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri wa wizara ya Nishati na Madini.
Baadhi ya waandishi na maofisa mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia maelezo ya kujiuzulu Waziri Prof. Sospeter Muhongo hii leo.
 **********
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri hii leo.

Prof. Muhongo ametangaza uamuzi huo asubuhi ya leo katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini.

Akitangaza uamuzi huo Prof. Muhongo amesema ameamua kuachia wadhifa huo ili kupisha nchi ijadili na kufanya mambo muhimu ya maendeleo badala ya kuendelea kujadili masuala ya Escrow.

"Wananchi wamechoka, na hata mimi mwenyewe nimechoka kila kukicha watu wanajadili ESCROW, hivyo anajiuzulu ili watu wafanye kazi na kuleta maendeleo," alisema prof Muhongo.

Aidha amesema sakata yeye anaendelea kusisitiza na kusimamia msimamo wake kuwa hahusiki kwa namna yeyote ile katika uchukuaji wa fedha za akaunti ya Escrow kama inavyodaiwa na watu.

Waziri huyo amejiuzulu ikiwa ni baada ya kuitumikia wizara hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tu, huku akiwa amefanya jitahada kubwa kuhakikisha wananchi vijijini wanapatiwa umeme kwa gharama nafuu. 

Muhongo amesema ni wakati mzuri sasa kuviachia vyombo vya dola hasa Mahakama kujadili suala la Escrow nasio watu wengine mitaani. 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates