UZINDUZI WA MSIMU WA 13 WA MBIO ZA KIMATAIFA ZA KILIMANJARO MARATHON ULIVYOFANA JUZI MJINI MOSHI.
Posted by
woinde
on
Saturday, January 31, 2015
in
MATUKIO
MICHEZO
|
|
Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa akiwa ameshika bendera kuashiria uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni,Uzinduzi uliofanyika Hotel ya Kibo Homes,Wengine ni Viongozi katika kampuni ambazo zimejitkeza kudhamini mbio hizo |
|
Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni,Uzinduzi uliofanyika Hotel ya Kibo Homes, |
|
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli ambao ndio wadhamini
wakuu wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2015 ,akizungumza wakati wa
uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio hizo uliofanyika Hotel ya Kibo Homes
mjini Moshi. |
|
Baadhi ya wageni walikwa katika uzinduzi wa msimu wa 13 wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni uliofanyika mjini Moshi. |
|
Mkurugenzi
wa Kanda ya kaskazini wa kampuni ya Tigo Tanzania ,David Charles ambao
ndio wadhamini wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni kilometa 21 akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika mjini Moshi. |
|
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Mafuta na vilainishi GAPCO ,Caroline Kakwezi ambao
ndio wadhamini wa mbio za watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa
uzinduzi wa mbio hizo. |
|
Mwenyekiti
wa chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Methacha
akizungumza wakati wa hafla ya fupi ya uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio
za Kilimanjaro Marathoni. |
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kibo Palace Hotels na Kibo Homes ,Vicent Lasway akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika katika Hotel ya Kibo Homes. |
|
Wanariadha toka klabu ya riadha ya Holili wakifuatilia uzinduzi hhuo. |
|
Baadhi ya viongozi walioalikwa katika uzinduzi wa mbio hizo. |
|
Mkurugenzi
wa kampuni ya ExecutiveSolution ,Aggrey Mareale akitoa maelezo mafupi
kuhusiana na mbio za Kilimanjaro Marathoni ambazo zimeingia msimu wa 13
,zitakazofanyika mwezi wa tatu mwaka huu. |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia