Mwezeshaji wa Semina juu ya
HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
Bw.Zachariah A.Babu akiwa anatoa maelekezo kwa waandishi wa habari juu
ya Haki ya watoto

Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kuwasilisha masuala yanayowahusu
watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. Akizungumza na
wanahabari kutoka vyombo mbalimbali jijini Arusha katika warsha juu ya
HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoendeshwa na shirika liliso la kiserikali la The Foundation For
Tomorrow (TFFT),
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania wa shirika hilo,
Bwa. Kennedy Oulu alisema tatizo la watoto yatima na wale waishio
katika mazingira magumu nchini Tanzania ni gumu, hivyo vyombo vya habari
havina budi kuifahamisha jamii kuhusu hili suala na matatizo
yanayowakabili watoto yatima na waishio katika mazingira magumu ili
jamii na wadau mbalimbali waweze kushiriki vema katika kukabiliana na
tatizo hili.
“Kwa sasa, inakadiriwa kuwa kuna watoto
yatima na wale waishio katika mazingira magumu wapatao 1,800,000 hapa
Tanzania pekee, huku 1,300,000 kati yao wakiwa wametokana na athari za
ugonjwa wa UKIMWI. Mgawanyo wa kifamilia na muundo wa kimsaada kijamii
ni moja ya vinavyochangia tatizo hili. Vinapoongezwa katika umaskini
unaojidhihirisha katika: ukosefu wa upatikanaji wa huduma za elimu
ikiwemo elimu ya awali, ukosefu wa upatikanaji wa huduma za afya na
uzalishaji kama afya ya uzazi, ukosefu wa stadi za maisha zinazoakisiwa
katika mitaala ya shule zenye uwezo unaotakiwa na ubunifu ili kujenga
uwezo wa watoto, si kwa yatima na waishio katika magumu pekee”. Alisema
Kennedy na kuongeza
“Ni muhimu kutambua kuwa kumekuwa na hatua
na mafanikio yaliyofikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali katika
kuwezesha upatikanaji, kuzijengea uwezo familia za watoto hawa na
kubadili mitazamo ya jamii dhidi ya watoto yatima na wale waishio katika
mazingira magumu, hii inajenga msingi wa mwitikio endelevu.
Kwa upande wake, shirika la The Foundation For Tomorrow limekuwa
likilishughurikia tatizo hili kwa njia mbalimbali. Shirika hili hutumia
njia anuai ambazo hupunguza uhitaji wa watoto yatima na wale waishio
katika mazingira magumu kwa kuzijengea uwezo wa kiuchumi kaya zao
hususani zile kaya maskini kupindukia, kutoa msaada wa kugharamia masomo
ili kuwahakikishia upatikanaji wa elimu, kutoa bima za afya kwa
wanafunzi yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu, kuwajengea
uwezo walimu na kuwezesha stadi za maisha kwa njia ya kuboresha mtaala.
Bwa. Oulu amesema juhudi hizi pamoja na sauti za watoto yatima na wale
waishio katika mazingira magumu zinapaswa kufahamika. “Changamoto za
hawa watoto na mitazamo yao hutusaidia kutambua njia iliyo bora ya
kulinda maisha yao. Hizo pia hutuwezesha kutambua kuwa kwa kiasi kikubwa
sote tunalo jukumu la kubadili vile tunavyowachukia hawa watoto kutoka
katika kudharauliwa na badala yake kuwa katika ufahamu kuwa sababu ya
hali hizo na magumu yaliyopo ndiyo matatizo tunayoyashughurikia Tanzania
yote: elimu, afya, umaskini, kaya na kufikia fursa zilizopo.”
Inapaswa kuoneshwa ya kwamba hali hii lazima
ionwe kuwa si ya kudumu wakati hatua zinazochukuliwa, kujenga kipato
baina ya kaya maskini, kuwezesha upatikanaji wa mahitaji na kulinda haki
na ulinzi kwa watoto, hususani kwa kuwahakikishia elimu bora na
ushiriki wao usio na kikomo ni muhimu katika kutokomeza tatizo hili.
Bwa. Oulu aliongeza kuwa “Uandishi wa habari
wa kiuchunguzi na uwasilishaji mambo wenye malengo, suluhisho, utendaji
bora na juhudi zilizoshindwa ndivyo vitaiwezesha jamii kujua ni njia
gani bora ya kusaidia, kuitikia na kudumisha juhudi na fursa za
kuwaondoa watoto yatima na wale wasiojiweza kutoka katika janga hilo.
Inapaswa ioneshwe kuwa watoto yatima na wale waishio katika mazingira
magumu pamoja na wanaowahifadhi na kaya zao wanayo hatua kubwa ya
kuchukua.”
Sambamba na hilo, msimamizi wa warsha hiyo Bwa. Augustine Zacharia alivishauri pia vyombo vya habari kuzingatia ni jinsi gani habari zinazotolewa katika vyombo vyao huwaathiri watoto hawa kwa upande chanya na hasi. Masuala yahusuyo watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu yanapaswa kuwasilishwa katika namna ambayo huwajenga na kuwa katika mtazamo wa kutafuta suluhisho la tatizo. Licha ya kuwa kuna uhuru wa kutoa na kupokea habari, lakini namna ambavyo habari hizi huwasilishwa, zinapaswa kwanza kuzingatia kuwa haki za watoto hazivunjwi.
*********************************************

KUHUSU THE FOUNDATION FOR TOMORROW.
The Foundation For Tomorrow huutazamia ulimwengu ambao watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu wanachangia katika jamii kama raia waliowezeshwa bila kubaguliwa, kuathiriwa, na uhitaji. Lengo la shirika hili ni kuhakikishia elimu bora na msaada wa kihisia kwa watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu ili waweze kufikia viwango vya juu kabisa vya uwezo wao na kushamiri katika jamii zao