Msanii wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba akiimba akapela moja ya
nyimbo zake wakati wa mkutano huo na wandishi wa habari (Hawapo
pichani), katika mkutano huo juu ya ushiriki wake kwenye tamasha hilo
linalotarajia kufanyika Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzibar.
kushoto kwake, ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf,
akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, Simai Mohammed.
**********
Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba
kukonga nyoyo watu mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la
Sauti za Busara linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome
Kongwe, Zanzubar.
Ali Kiba alieleza hayo leo Alhamisi, Januari 29. wakati wa
mkutano wa ulioandaliwa na Busara Promotions, wandaaji wa tamasha hilo
kubwa la Kimataifa linalofanya muziki wa ‘Live’, ambapo kwa mwaka huu
zaidi ya wanamuziki na vikundi 37, watatoa burudani kwenye tamasha hilo
kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari, Ali Kiba alisema kwa
sasa amejiandaa kutoa burudani ya aina na ambayo itakonga nyoyo kwa watu
wote watakaojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
“Hii itakuwa ni zawadi kwa watanzania wote kunishuhudia nikiimba
‘live’ bila kutumia ‘cd’ kama wafanyavyo wengine. Mimi ni mwanamuziki
na nimesoma muziki hivyo nitapiga muziki wa nguvu jukwaani” alisema Ali
Kiba.
Na kuongeza kuwa, kwa sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa
kujifua na bendi maalum kwa ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye
ni msanii kwani muziki aliusomea na kujifunza huko nyuma alipokuwa
katika Nyumba ya kuibua vipaji THT, ambapo alijifunza vitu vingi
ikiwemo kuimba muziki wa bendi na ‘live’.
Aidha, aliwaomba wapenzi na wadau wa muziki kujitokeza kwa
wingikushuhudia tamasha hilo kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje
watatoa burudani ya kipekee.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Busara Promotion,
wandaaji wa tamasha hilo, Simai Mohammed, alisema tamasha limeweza
kuongeza ajira na uchumi wa Zanzibar kwani pia limeongeza fursa za
utalii.
Kwa upande wake, Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani,
alisema tamasha hilo limeweza kuongeza fursa kila mwaka ikiwemo kutoa
ajira kwa vijana wa kitanzania kwa asilimia 90, ambapo kwa mwaka huu
wanatarajia kuwa na watendaji kazi na wa kujitolewa watakolipwa katika
kusaidia tamasha hilo, zaidi ya watu 150.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud
‘Dj Yusuf’ alisema tamasha hilo limeweza kuibua wasanii mbalimbali
ikiwemo kujitangaza kimataifa.
Aidha, Dj Yusuf alieleza kuwa, tamasha la mwaka huu litaendana
na kauli mbiu ya kuimiza Amani, pia wameandaa tuzo maalum na zawadi
maalum kwa wasanii wa Tanzania watakaoshinda katika kutunga nyimbo za
amani.
Mbali na Ali Kiba, Wasanii wengine Isabel Novella kutoka
Msumbiji, Ihhashi Elimhlophe (Afrika Kusini), Tcheka (Cape Verde),
Diabel Cissokho (Senegal), Culture Musical Club (Zanzibar), Msafiri
Zawose (Tanzania), Aline Frazão (Angola), Tsiliva (Madagascar),
Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band (Tanzania), Mohamed Ilyas &
Nyota Zameremeta (Zanzibar), Thaïs Diarra (Senegal / Mali / Uswisi),
Liza Kamikazi and band (Rwanda), Erik Aliana (Cameroon), Mpamanga
(Madagascar), Mgodro Group (Zanzibar), Rico Single & Swahili
Vibes (Zanzibar), Zee Town Sojaz (Zanzibar), Ifa Band (Tanzania) na
wengine wengi.