Watu wenye
ulemavu nchini wameiomba serikali na taasisi binafsi zinazotoa huduma za
kijamii ikiwemo hospitali,benki na shule kuhakikisha kuwa wanaweka miundombinu rafiki
itakayowawezesha kuzifikia huduma hizo kwa urahisi.
Katibu wa
Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu Arusha ,Yunusi Urasa amesema kuwa
kumekua na tatizo la la kukosekana kwa miundombinu rafiki kwa walemavu hali
inayowakwamisha kupata huduma hizo muhimu kutokana na ulemavu walionao.
Yunusi
aliyasema hayo jana katika semina ya watu wenye ulemavu iliyofanyika jijini
Arusha na kuandaliwa na Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu nchini ,ambapo amesema kuwa amehimiza serikali
kuwakumbuka walemavu katika upangaji wa miji,ujenzi wa barabara na majengo ili
waweze kupata haki zao za msingi za kunufaika na huduma za jamii.
Katibu huyo
amependekeza kuwepo kwa dawati maalumu la kuwahudumia watu wenye mahitaji
maalumu litakalowasaidia walemavu kupata huduma kwa urahisi.
“Mlemavu
asiyeona akienda benki hawezi kutumia
ATM card ni rahisi kuibiwa akikutana na mtu ambaye si mwaminifu,pegine
zitengenezwe ambazo wataweza kuzisoma
pia ATM ziko juu kwa walemavu wanaotambaa ni vigumu kuzifikia” Alisema
Yunusi
Naye Katibu wa
Chama cha Watu wenye ulemavu wa ngozi Arusha Happiness Raphael amesema kuwa
wanashangazwa kuona mauaji ya albino yanaendelea huku mashirika ya haki za
binadamu ya kimataifa yakikaa kimya hivyo ameiataka jamii ya kimataifa kuchukua
hatua kukomesha vitendo hivyo.
Mratibu wa
Shirikisho la Watu wenye Ulemavu nchini Francis Mhina amesema kuwa wanafanya
juhudi za kutoa elimu kwa walemavu juu haki zao za msingi na namna ambayo
wanaweza kujikwamua kimaisha ,ameeleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni uhaba wa fedha hivyo
kushindwa kuwafikia walemavu wengi ambao wako vijijini na kuishia mijini.