Mamlaka ya
chakula na dawa kanda ya kaskazini TFDA, imefunga ghala la vipodozi bandia(feki)
lililoko mafichoni katikati ya makazi ya watu jijini Arusha,na kisha kuteketeza
shehena hiyo ya vipodozi hivyo.
Mamlaka ya chakula na dawa ilifanya ukaguzi wa kushutukiza,na kukuta limesheheni ghala
hilo limesheheni vipodozi bandia vilivyopigwa
marufuku kuingizwa nchini.
Ukaguzi huo
wa kushutukiza umefanyika juzi Januari 14,baada ya mamalaka ya chakula na dawa
TFDA, kupata taarifa za siri za kuwepo ghala la vipodozi bandia kwenye makazi
ya watu eneo la mita 200 jijini Arusha.
Akizungumza
wakati wa zoezi la kuteketeza bidhaa hizo kwenye Jalala kuu la halmashauri ya
jiji la Arusha, lililopo eneo la Mriet kata ya Sokon one ,meneja wa TFDA, kanda
ya kaskazini Damas Matiko, amesema bidhaa hizo ambazo zina thamani ya shilingi
milioni 7 zilizoteketezwa hazikusajiliwa kwa soko la Tanzania.
Zoezio hilo
la kufunga ghala hilo limefanyika chini ya ulinzi wa jeshi la polisi baada ya TFDA,kupata taarifa za siri na hivyo
kunyata na kulikuta ghala hilo likiwa na bidhaa hizo zenye uzito wa tani 2 ambazo ni vipodozi vilivyopigwa marufuku
kuingizwa nchini na katika upekuzi huo
kulikutwa shehena hiyo ya bidhaa hizo zisizofaa kwa matumizi ya binadamu
.
Matiko ,
amesema kuwa ghala hilo limekutwa mafichoni eneo la mita 200 kwenye makazi ya
watu katika jiji la Arusha, ambapo bila taarifa sahihi huwezi kufahamu kama
kuna ghala tena lililosheheni vipodozi .
Amesema
ghala hilo lipo kwenye nyumba ya mtu ambapo hutumika kuhifadhia bidhaa hizo za
vipodozi, ambapo huwa inahamishwa kidogo kidogo kupelekwa kwenye maduka
kulingana na mahitaji .
Matiko,amesemja
TFDA, itaendelea kusimamia utekelezaji wa lengo lake la kulinda na kuokoa afya za walaji ili
kuwaepusha kupata maladhi mbalimbali yakiwemo kansa, athari za ngozi, mwili,
viungo vya uzazi mfumo wa damu kuathiri ubongo na makuzi ya watoto.
Ameongeza
kuwa lengo lingine la TFDA ni kuondoa bidhaa zote ambazo hazikusajiliwa kwa
soko la Tanzania kwenye maduka ili ibakie bidhaa zinazotakiwa tu .
Amesisitiza
kuwa ni lazima wafanyabiashara wafuate taratibu kwa kuingiza bidhaa
zinazoruhusiwa kwa soko la ndani ambazo zimesajiliwa na TFDA ,ambazo lugha na
maelezo yake ni ya Kiingereza na kiswahili tu, na si vinginevyo.
Kwa upande
wake Afisa afya kutoka jiji la Arusha, Angela Mogitu, amewatahadharisha wanawake
kuepuka kutumia vipodozi ambavyo hawavifahamu
kwa kuwa vinawasababishia madhara makubwa .
Mogitu,
amesema vipodozi vyote vilivyopigwa marufuku vina madini ya Zebaki ambayo ni
hatari kwa afya ya mtumiaji pia huharibu
mfumo wa uzazi na damu na ngozi hivyo
wasivitumie madhara yake ni makubwa.
Mimiliki wa
ghala hilo,Deo Simon Mwacha (32)ambae
pia anamiliki duka la kuuza vipodozi katika mtaa wa Mnazi mmoja jijini Arusaha,
amekiri kuingiza bidhaa hizo na kudai kuwa huwa ananunua katika maduka makubwa
ya vipodozi jijini Dar es Salaam.
Macha amesema
amekuwa hununua vipodozi hivyo na kuviuza kwa wateja mbalimbali dukani kwake lakini hakujua kama vina madhara .
Mara baada
ya kutiwa nguvuni mtuhumiwa huyo akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi alipakia
bidhaa zake kwenye gari lake Toyota Noah,hadi jalala kuu la Arusha lililopo
eneo la Mriet kata ya sokon one na kuishusha kisha akishuhudia ikiteketezwa kwa
moto na mamlaka ya chakula na dawa TFDA.