Naibu
waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akikabidhiwa ua na
mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Christina Nyenga wakati wa
mapokezi ya Naibu Waziri jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah
Kairuki (kulia) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Ummy Mwalimu wakati akimkabidhi ofisi jijini Dar Es Salaam .
kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri lililofanyika Jumamosi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah
Kairuki akimkabidhi nyaraka mbalimbali Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba
na Sheria Bi. Maimuna Tarishi wakati Mhe. Kairuki alipokuwa akikabidhi
ofisi jijini Dar Es Salaam.