Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akimwelezea Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel
Kristian Kileo (wa pili kushoto), namna mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa
ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa zinazotokana na
mifugo kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za Wilaya ya
Ngorongoro
utakavyotekelezwa juzi katika Kijiji cha Ololosokwan.
Wengine ni maofisa miradi kutoka UNESCO wakishuhudia. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akimwelezea Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel
Kristian Kileo (wa pili kushoto), namna mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa
ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa zinazotokana na
mifugo kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za Wilaya ya Ngorongoro
utakavyotekelezwa juzi katika Kijiji cha Ololosokwan. Wengine ni maofisa
miradi kutoka UNESCO wakishuhudia.[/caption]
SHIRIKA la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini Tanzania linatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa kituo
cha sanaa ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa
zinazotokana na mifugo kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za
Wilaya ya Ngorongoro kama jitihada za kuongeza kipato kwa familia za jamii
ya Wamasai.
Akitoa maelekezo ya mradi huo juzi katika Kijiji cha Ololosokwan mbele ya
Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo,
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues alisema mradi huo unatarajia kutekelezwa
kuanzia Mwezi Agosti, 2015.
Bi. Rodrigues alimueleza Kileo kuwa mradi huo unajumuisha ujenzi wa kituo
cha kisasa cha sanaa ambacho kitatumiwa na wajasiliamali wa jamii ya
Kimasai kwa ajili ya kuuza bidha zao za asili mbalimbali kwa watalii
wanaofika kutembelea vivutio anuai vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya
Ngorongoro inayozunguka vijiji hivyo.
Akifafanua zaidi juu ya mradi huo, Ofisa Mradi Utamaduni wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Rehema
Sudi alisema mradi huo utajumuisha mafunzo ya ujasiliamali juu ya
utengenezaji wa bidhaa za ngozi, pembe za ng'ombe pamoja na shanga ili
kuziongezea thamani na kuuzwa kwa watalii anuai wanaotembelea vivutio na
kukuza vipato vya familia hasa akinamama.
Bi. Sudi aliongeza kuwa kata zinazotarajia kunufaika na mafunzo na ujenzi
wa kituo hicho cha kisasa kwa ajili ya mauzo ya bidhaa hizo za asili za
Wamasai ni pamoja na Kata za Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili na
Kata ya Aoliani Magaidulu zote za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
"...Mradi huu utajumuisha akinamama na wasichana kutoka kata tano ambazo ni
Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili na Kata ya Aoliani Magaidulu,
tutawapatia mafunzo juu ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana
na ngozi na pembe za ng'ombe pamoja na shanga ikiwa ni hatua ya kuziongezea
thamani kisha kuziuza kwa watalii ambao wanatembelea vivutio vya utalii
eneo hili hasa Kijiji cha Ololosokwan," alisema Ofisa Mradi Utamaduni
Unesco, Bi. Sudi. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akimuonesha Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel
Kristian Kileo (wa pili kulia) kompyuta ndogo mpakato ambazo zimefungwa
katika darasa moja maalumu kwa mafunzo mbalimbali kwa watoto na wahitaji
wengine. Darasa hilo ni sehemu ya mradi wa kidijitali unaojumuisha Kliniki
ya kisasa ya matibabu
ya macho na meno pamoja na huduma za uchunguzi
magonjwa mbalimbali kwa kutumia fipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra-sound' na
shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akitembelea eneo la mradi wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha Kliniki ya
kisasa ya matibabu ya macho na meno pamoja na huduma za uchunguzi magonjwa
mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na shule ya
kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Katikati ni Katibu Tawala,
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo pamoja na Ofisa
Mradi Utamaduni wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania, Rehema Sudi wakikagua
mradi huo. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akitembelea eneo la mradi wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha Kliniki ya
kisasa ya matibabu ya macho na meno pamoja na huduma za uchunguzi magonjwa
mbalimbali kwa kutumia fipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na shule ya
kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Katikati ni Katibu Tawala,
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo pamoja na Ofisa
Mradi Utamaduni wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania, Rehema Sudi wakikagua
mradi huo.[/caption]
[caption id="attachment_58717" align="aligncenter" width="800"] Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha
kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno,
huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray'
na 'Ultra- sound' na shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini
hapo. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine
ikiwemo kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani
Ngorongoro.[/caption]
Alisema wataalam na wabunifu wataletwa katika vijiji vya mradi na kutoa
mafunzo kwa akinamama na wasichana kabla ya ujenzi wa kituo maalumu ambacho
kitatumiwa na wanufaika wa mafunzo hayo kama eneo la kuuzia bidhaa zao
ikiwa ni sehemu pia ya kulinda na kukuza tamaduni za jamii ya Wamasai.
"...Tutazunguka na kutoa mafunzo juu ya ubunifu na utengenezaji wa bidhaa
mbalimbali za ngozi, pembe za ng'ombe pamoja na shanga na kutengeneza
bidhaa za asili kwa ajili ya kuziuza kwa wateja hasa watalii," alisema Bi.
Sudi.
Hata hivyo Ofisa huyo mradi Utamaduni wa UNESCO alisema sehemu ya
maandalizi ya mradi huo unaotekelezwa kwa msaada wa UNESCO pamoja na
washirika wengine ambao ni Umoja wa Ulaya (EU) na Chuo Kikuu cha
Liechtenstein na pia Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar es Salaam imeanza
kutekelezwa tangu Februari 2015.
Mbali na mradi huo UNESCO pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa Kijiji cha
Dijitali, ambao unajumuisha ujenzi wa Kliniki ya kisasa ya matibabu ya
macho, Kliniki ya kisasa ya matibabu ya meno pamoja na huduma za uchunguzi
wa magonjwa mbalimbali kwa kutumia fipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra-sound' na
shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai katika Kijiji cha Ololosokwan
huduma itakayosaidia jamii za wafugaji maeneo ya Ngorongoro. Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha
kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno,
huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray'
na 'Ultra- sound' na shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini
hapo. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine
ikiwemo kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani
Ngorongoro. Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha
kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno,
huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray'
na 'Ultra- sound' na shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini
hapo. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine
ikiwemo kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani
Ngorongoro.[/caption]
[caption id="attachment_58716" align="aligncenter" width="800"] Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha
kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno,
huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray'
na 'Ultra- sound' na shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini
hapo. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine
ikiwemo kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani
Ngorongoro Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha
kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno,
huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray'
na 'Ultra- sound' na shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini
hapo. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine
ikiwemo kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani
Ngorongoro.**Imeandaliwa na www.thehabari.com ,*
Ngorongoro
___________________________________________