MADUKA TISA YA BIASHARA JIJINI HAPA YAUNGUA MOTO

 Moto uliteketeza maduka mengi


 wengine walijaribu kuokoa vitu vilivyokuwa madukani mwao


 Zimamoto wakishirikiana na wananchi walijitahidi sana kuzima moto huo




Mashuhuda nao hawakukosekana walijitokeza kwa wingi kuangalia moto huo


 moshi ulitanda  kila mahala


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida maduka tisa ya biashara jijini hapa yameungua moto na kusababisha hasara ambayo mpaka sasa haijafahamika , hali ambayo imesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara

Wakizungumza na “libeneke ” jana  mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa moto huo ulianza majira ya saa tisa za mchana  katika moya ya maduka ambapo walianza jitiada za kuzima moto huo bila mafanikio yoyote

Mashuhuda hao waliongeza kuwa maduka hayo ambayo  yapo katika eneo la Mtaa wa majengo yaliendelea kutapakaa kwa moto kwa muda huku moto huo ukiendelea kuleta madhara makubwa ikiwemo kuunguza sana bidhaa ambazo zilikuwa zinauzwa katika maduka hayo.

“kwa kweli tulijarib kwa kiasi kikubwa kuzima moto ule ile usiendelee kutapakaa katika maduka mengine lakini baada ya hapo tulifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana na  ndipo baada ya muda mfupi kikosi cha kuzima moto na chenyewe kilifaka ili kuokoa maduka hayo 9 ambayo chanzo mpaka sasa hatujajua nini”

Hataivyo waliongeza kuwa mara baada ya kupata msaada kutoka kwa kikosi hicho waliendelea na kazi ya kupunguza makali ya moto huo lakini baadaye maji yaliisha  hali ambayo ilizua tafrani kubwa sana

Katika hatua nyingine wananchi hao waliiomba serikali kuweza kuboresha huduma za Zima Moto kwa jiji la Arusha ambapo mara nyingi sana wanaishiwa na dhana za kufanyia kazi

“ni aibu sana kwa kikosi kama hii kukosa  maji nah ii sio mara moja imeshajitokeza hata kwenye majanga mengine ya moto kwa hali hiyo basi inatakiwa kuangalia sana kwa kuwa bado Serikali ina uwezo mkubwa sana  wa kufanya hivyo”waliongeza wananchi hao

Walifafanua kuwa Serikali inatakiwa kuangalia kwa undani sana suala hilo kwa kuwa wao ni watu wa Muhimu sana kuliko sekta yoyote ile kwa kuwa mara nyingi sana wanaokoa maisha ya watanzania hasa kwenye majanga ya hatari kama majanga ya moto

Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani hapa bw Akili  Mpwapwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi unaendelea juu ya tukio hilo la moto ambapo mpaka sasa bado chanzo hakijafahamika.

habari hii imeandikwa na  QUEEN LEMA wa libeneke la kaskazini

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post