Tatizo la kutojua kusoma na kuandika
kwa baadhi ya wananchi wa kata ya Kingori pamoja kata ya Leguruki limesababishia
zoezi la kupiga kura kuwa gumu
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wasimamizi wa vituo vilivyopo katika kata
hizo wakati wakiongea na nipashe katika vituo vyao
Akiongelea tatizo hilo msimamizi wa kituo cha zahanati yangejisesia alisema
kuwa zoezi hilo limekuwa gumu kwao kwani wapiga kura wengi ambao wanaenda katika
vituo vyao wamekuwa hawajui kusoma na kuandika hivyo wamekuwa wakipata shida
sana kuwasaidia.
"kwakweli swala la kusoma na kuandika ni tatizo kubwa kwani vijana
wazee,kwa ufupi kuna watu wa rika mbalimbali wanakuja hapa hawakui kusoma na
kuandika ivyo sisi tunawasiaidia kwanza tunawaambia kama wana mtu ambaye
anamwamini aje naye na kama hana ndo inabidi tatafute njia mbadala"alisema
Msimamizi wa shule ya sekondari King'ori ambaye hakutaka kutaja jina
Alisema kuwa pia ukiondoa kusoma na kuandika pia elimu inatakiwa itolewe
kwa wananchi kabla ya kupiga kura kwani kuna baadhi ya wananchi wamekuwa
wakienda kupiga kura huku wakiwa hawajui sheria za uchaguzi
Kwa upande wake msimamizi mungine aliyekuwa akisimamia kituo cha shule ya
msingi Malula ambapo katika shule hii inavituo vitatu mmoja wa wawasimamizi wa
kituo vituo hicho ambaye yeye alikuwa anasimamia kituo cha pili Aginess
Pallaanjo yeye alisema kuwa katika kituo chake wamekuwa na tatizo la wananchi
wengi kwenda katika kituo hicho bila ya kuwa na kadi ya kupiugia kura huku
majina yao yakiwa yapo na wao kama wasimamizi wa vituo wamekuwa wakipata tabu
saba kuwaelimisha watu hao mpaka wakakubali kuondoka katika vituo vyao bila ya
kupiga kura.
Aidha alibainisha kuwa pia katika kituo kumekuwa na tatizo la kutokuwepo na
kitabu No.15540 kitabu ambacho kinatumika kuhakiki maelezo ya mpiga kura hali
inayopelekea mpiga kura mungine kushindwa kupiga kura kwani amekuwa anaonekana
na kitambulisho lakini jina lake halionekani huku katika sehemu zingine wapiga
kura wengine wakiwa wanakadi lakini kwenye kitabu chao kunaonekana namba ya kadi
haziendani na ya kitabu.
Gazeti hili la Nipashe lilishuhudia ulinzi ukiwa umzuri katika vituo hivi
na kila kituo cha kupigia kura kulikuwa na askari polisi wawili waliokuwa
wakilinda ulinzi katika eneo husika huku baadhi ya magari ya polisi
yakionekana kuzunguka katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kulinda fujo
zisiweze kutokea
Wakiongelea uchaguzi huu baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura
walisema kuwa uchaguzi huu ni wa kihistoria kwani wananchi wengi wa vijijini
haswa kata hii wamejitokeza kwa wingi kupiga kura pia walipongeza ulinzi
uliowekwa kwani upo vizuri na makini sana.
''kwakweli uchaguzi wa mwaka huu kipindi hichi hatujawai kuona kwani watu
wamejitokeza na wanazidi kuja kingine kinafurahisha ni ulinzi kweli ulinzi
umeimarishwa sana kwanza tangu kampeni ziaze yaani ata wezi na vibaka
tumewasahau kwani kunaulinzi wa kutosha afu kingine huu ulinzi wa kituo kwa sasa
ni mzuri maana sidhani ata kama fujo itatokea wala vurugu kama zinavyotoke aga
katika chaguzilizopita "alisema Lukasi Nikinyi Laizer
Vituo hivi vya kupigia kura
vimefunguliwa mapema kuanzia saa moja kamili asubuhi nawananchi wameanza
kujitokeza kwa wingi kuanzia saa mbili kamili asubuhi huku adri muda ulivyo zidi
kwenda ndo walivyozidi kuongozeka kwani wengi wao walikuwa wametoka