MWENYEKITI CCM AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 12


MWENYEKITI wa CCM Tawi la Kairo Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya
Simanjiro Mkoani Manyara ambaye anatumikia hukumu ya kifungo cha nje
cha miezi 12 ametangaza nia ya kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi
ujao wa chama hicho.

Mwenyekiti huyo Safiel Saitore alihukumiwa kifungo hicho na Mahakama

ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya mkoa huo,kwa kosa la
shambulio la kudhuru mwili alisema atajitosa kwenye kinyanganyiro
hicho.

Akizungumza
 na waandishi wa habari,Saitore ambaye alihukumiwa
kifungo hicho mwishoni mwa mwaka jana kwa kumpiga Ofisa Mtendaji wa
kata ya Mirerani alisema wapinzani wake wanawadanganya watu kuwa
hatagombea sababu ya hukumu hiyo.

Alisema baadhi ya watu wanaoitaka nafasi hiyo wanawalaghai wanachama

wa Tawi la Kairo kuwa hatatetea nafasi yake kutokana na yeye kutumikia
adhabu ya hukumu ya kifungo cha nje hivyo nafasi hiyo itagombewa na
watu wengine.

Aliwashauri wanachama hao wanaoeneza maneno hayo waende darasani kwa

ajili ya kujifunza siasa ili waitambue katiba ya CCM kwani ameipitia
yote na hajabaini mahali ambapo katiba hiyo imemkataza kugombea nafasi
hiyo.
  "katiba ya CCM ukurasa wa 11,ibara ya 13 (1) ‘a’ mpaka ‘e’
inasema uanachama utakishwa kwa kujiuzulu mwenye,kuachishwa kwa mujibu
wa katiba na kufukuzwa kwa mujibu wa katiba hilo kwangu silitambui sasa watu wanatakiwa kusoma katiba na kuielewa na sio kukurupuka" alisema



Alisema endapo angekuwa anagombea nafasi ya kuwakilisha chama kwenye

Serikali katika nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali,Diwani au Mbunge
ndiyo kungekuwa na tatizo,lakini kugombea nafasi ndani ya chama hakuna
tatizo.

Hata hivyo,alisema hakuridhika na hukumu ya kesi hiyo iliyotolewa

dhidi yake na Mahakama ya Hakimu wa mkoa wa Manyara na ameshakata
rufaa kwenye Mahakama Kuu kanda ya Arusha na imeshapangiwa jaji wa
kusikiliza.

Amewataka wanachama wa CCM tawi la Kairo wanaotaka kugombea nafasi ya

Uenyekiti wapime kifua chao kama watahimili mapambano waingie ulingoni
kuliko kusambaza maneno yenye kupotosha ukweli kwa wanachama.

Alisema kuwa baadhi ya wanachama wa tawi hilo badala ya kujipanga na

kulipa ada ya uanachama wanalalamikia nafasi yake na kushindwa kutoa
hoja ya msingi na kusimamia hoja mfu ambayo haipo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post