Aliyekuwa mwenyekiti wa Uvccm Jemsi Ole Millya akionge na waandishi wa habari
MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa Arusha,kwa miaka mitano, James Millya,
ametangaza kujiuzulu nafasi zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza
kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai
kuwa CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.
Aidha alisema hawezi kuendelea kupanda gari lenye pancha lukuki, hivyo
ameamua kupanda gari lisilo na pancha na lenye kutoa matumaini mapya
kwa watanzania Chadema.
Hayo aliyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye
Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini hapa.
Alisema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa
chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama
hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.
“Mimi nanukuu maneneo ya Nyerere kuwa alishawahi kusema CCM sio mama
yangu na mimi pia CCM sio mama yangu na natangaza rasmi, kuondoka
ndani ya chama hiki na najiunga Chadema, sababu ndicho chama chenye
kuleta tumaini jipya kwa watanzania,”alisema.
Alitaja nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya
utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe
Halmashauri Kuu CCM Mkoa.
ALisema kuw ainasikitisha kuona Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa
matamko kuwa Rais ajaye 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini na
anayemfahamu ni Rais peke yake ambaye ni Jakaya Kikwete.
Millya alisema cha kusikitisha pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na
hadi sasa Ikulu haijawahi kutoa kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza
kauli hizo kutolewa, jambo lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kw
anamna moja au nyingine na kauli hiyo.
Aidha alisema kuna Vijana wengi walioko ndani ya CCM wakiishi kw
amatumaini ya kusubiri kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio
Mkoa, ila yeye hawezi kuishi kw amatumaini kama muathirika wa Ukimwi.
Hata hivyo alitoa wito kwa Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi
mema ya nchi yao, kumfuata Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la
maisha ya watu.
Millya ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM tangu 2008 hadi
sasa, aliwashukuru vijana kw akumpa ridhaa hiyo na ataendelea
kuwashukuru, ila ameamua kwa ridhaa yake kuachia ngazi zote kwa ajili
ya ukombozi wa kweli.
Millya hivi karibuni alijitosa kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge wa
Afrika Mashari ndani ya Chama chake cha CCM, lakini alichinjiwa
baharini na kutolewa jina lake.
Wakati Kiongozi huyo akitangaza kuachia ngazi hiyo ya juu ya UVCCM,
ndani ya Chama cha CCM, Mkoa wa Arusha, Vijana mbalimbali wameonekana
kutoamini walichosikia na wengi wao wakionyesha nia ya kumfuata.
Akizungumza kwa niaba ya vijana wenzake, Hamisi Bakari, alisema kuwa
amesikitishwa na kiongozi wake kuhama chama na hiyo inaonyesha CCM
imeoza na hivyo kilichobaki hata wao kumfuata anakokwenda.
“Mimi na wenzangu tutakwenda huko aliko kwa sababu kama yeye kiongozi
ameamua kujiunga Chadema hata sisi wadogo hatuna mana ya kuendelea
kubaki huku,”alisema.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia