KAMPUNI ya uwakala wa kukushanya
ushuru wa magari madogo ya jijini Arusha, Kilimanjaro Millenium Printers
Limited (KMPL),imetoa siku 30 kwa halmashauri ya
jiji la Arusha iwe imeilipa deni la shilingi milioni 24 ,baada
ya manispaa hiyo kwenda kinyume na makubalinao ya mkataba na
kuisababishia hasara kubwa kampuni hiyo .
Kwa mujibu wa barua ya Kilimanjaro
Millenium Printers Limited iliyoandikwa machi 15 mwaka huu, kwenda kwa
mkurugenzi wa manispaa ya Arusha,yenye kumbukumbu namba KMPLDC/2012/02/15
inamtaka mkurugenzi huyo kulipa deni hilo la sh,milioni 24 ndani ya siku 30, na
baada ya muda huo kupita manispaa hiyo itaburuzwa
mahakamani.
Barua hiyo ilisema kuwa kampuni ya
KMPL iliingia mkataba na manispaa oktoba 10 mwaka 2011, kukusanya ushuru wa
magari madogo katika kituo kidogo cha daladala ikiwa ni pamoja na magari ya
Tours& shuttle(magari ya kukodi yanayosafirisha wageni).
Mkurugenzi wa KMPL,Thomas Munis
alisema kuwa kampuni yake nimeiandikia barua mara kadhaa
halmashauri hiyo ya kuikumbusha juu ya hasara inayoipata kwa siku
ambayo ni shilingi 200,000, kutokana na magari ya utalii kugoma
kulipa ushuru kwa shinikizo la manispaa hiyo kwa zaidi ya miaka
miwili sasa tangu oktoba mwaka 2011.
Alisema kuwa manispaa hiyo imekuwa
ikikaa kimya ikipuuza madai hao bila kutoa ufafanuzi ilihali inatambua wazi kuwa
kampuni hiyo imekuwa ikiingia hasara,hivyo kusudio la kampuni yake ni kuifikisha
mahakamani manispaa hiyo mara baada ya muda wa
notisi iliyoitoka kupita.
utashindwa kulipa deni hilo
mapema kampuni yangu itawajibika kuchukua hatua kali za kisheria ikiwa pamoja na
kukufungulia shauri la madai mahakamani kudai haki zetu ’’ilisema sehemu ya
barua hiyo.
Munis aliongeza kuwa kampuni yake kwa
sasa haipo tayari tena kuendelea kuilipa manispaa hiyo kupitia fedha zake za
mfukoni kwani hatua hiyo inatishia uhai wa kampuni yake kufilisika kutokana na
ukiukwaji wa mikataba inayofanywa holela katika manispaa hiyo bila
kushirikisha wataalamu wake.
Wakizungumza baadhi ya
madiwani katika halmshauri hiyo wameeleza kuwa,halmashauri hiyo huenda
ikafilisika kutokana na kuandamwa na kesi lukuki za madai kutoka kwa wakala
wale zinazotokana na ukiukwaji wa mikataba.
Diwani mmoja kupitia CCM ,ambaye
aliomba jina lake kutotajwa gezetini amedai kuwa manispaa hiyo imekuwa
ikiongozwa kihuni na kuingia mikataba mibovu na wakala bila hata kamati za
madiwani zilizoundwa ,kwani hali hiyo imekuwa ikitokana na baadhi ya watumishi
wa manispaa hiyo kujali maslahi binafsi zaidi na kuruhusu mikataba
isiyofaa.
Aliongeza kuwa manispaa hiyo imekuwa
ikifikishwa mahakamani mara kwa mara na wakala wake wanaoshinda tenda za
uwakala, baada ya kubainika kuwa manispaa hiyo imekiuka mkataba
iliyosainiwa.
Naye Naibu mkurugenzi wa manispaa ya
jiji la Arusha,Estomih Changa’h alipohojiwa alisema kuwa manispaa
hiyo inampango za kuzikutanisha pande zinazovutana ikiwemo chama cha
wasafirishaji utalii(Tato) ili kupata mwafaka wa suala hilo.
Akizungumzia suala la kudaiwa milioni 24 na
wakala wake ,alikiri kupokea barua ya madai hayo na kusema kuwa utatuzi wa suala
hilo unafanyika na hawategemei kama litafika kwenye vyombo vya
sheria.
‘’unajua hawakilimanjaro wanahangaika
bure ivi unadhani hizo fedha wanazodai ni za kuchukua tu kama unatoa fedha
mfukoni kwako,wewe waache wakifika mwisho watachoka ‘’alisema Changáh kwa
kifupi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia