Vongozi
wote ambao wameanza kuhama ndani ya chama cha mpinduzi wanakimbia kwa sababu
wamesoma alama za nyakati na kubaini kuwa katika uchaguzi uwa chama unaotarajia
kufanyika hivi karibu wamebaini kuwa hawatashinda.
Hayo yamesemwa na kada wa CCM mkoani hapa
ambaye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini wakati
akiongea na nipashe ambapo alidai kuwa hawa wanaotoka ni watoto wa magamba
ambayo chama hicho kilitangaza awali na kudai kuwa wajivue magamba mapema
Alisema kuwa viongozi hawa wa chama ambao
wameanza kujitoa katika chama wamejitoa kwa kuwa wamesoma alama za nyakati na
kuona kuwa katika uchaguzi wa chama unaokuja hawatapata nafasi za uongozi hivyo
wameamua kujitoa ili wajipatie jina na umaarufu kabla ya matokeo
Alisema kuwa wingi wao wanaojitoa walipata
fundisho katika uchaguzi wa Arumeru masharikia uchaguzi ambao mgombea
alichaguliwa na kikundi cha watu na sio chama ambapo walitumia fedha nyingi
lakini wakaambulia kupoteza jimbo
Aidha alisema viongozi hawa ambao wanajitoa
ndio ambao wameisabishia chama kuwa na mpasuko pamoja na makundi hivyo kujitoa
kwao kutasaidia kuondoa makundi yaliyopo katika chama hicho na kusabisha chama
hicho kuwa imara.
“jamani tukiangalia mfano mzuri kwa uyu
kiongozi wa UVCCM Jemsi Ole millya kwanza kabisa alikuwa ndio kiongozi anae
ongoza kwa kufanya fujo katika chama chetu na kabla yakujitoa kwake alikuwa
ameshapewa onyo kali ambapo katika onyo ilo ukirudi katika katiba
asingeruhusiwa kuchaguliwa nafasi yeyote katika chama na hata angegombea asingeweza
kupita na ndio maana jina lake lilikatwa katika uchaguzi wa ubunge wa Afrika
mashariki ivyo amejua kabisa itafikia maala ananafasi ya uongozi ndio maana
akaamua kuhama”alisema kada huyo
Aliongeza kuwa Mbali na ilo pia viongozi hawa
ambao wanatangaza kujitoa CCM katika kwa jina lingine aliwaita wanaojivua gamba
wengi wao wanamadhambi na walitakiwa kujitoa kabla ya uchuguzi huu
kufikia na kwa kuwa wamesoma alama za nyakati wakaziona ni mbaya ndio
maana wakaamua kujivua gamba huku wengine wakiwa wanajua muda wao umeisha wa
kuwa viongozi na wanatakiwa kuwaachia wengine wanaamua kujivua magamba yao.
“unajua hawa viongozi na pia napenda kumtolea
mfano huyu ambaye alianza kuonyesha njia kwakuwa yeye ndo alikuwa viongozi wa
vijana hapa mkoani Arusha ambaye naweza sema kuwa anauchu wa madaraka kwa kuwa
yeye baada yakukosa nafasi ya ubunge wa afrika mashariki ndo anaamia chadema na
kwanini asiamie uko kabla na pia kiongozi huyu bora ametutolea mzigo katika
chama chetu haswa mkoa wa Arusha kwani alikuwa ni sehemu ya migogoro na fujo
zilizokuwa zinafanywazo na vijana wa chama wilaya na hata mkoa “alisema kada
huyo.
Alisema kuwa jambo kubwa ambalo milya
alilalamikia kuwa ndio limemuuthi kuwa ni vijana wa ccm pwani kusema kuwa rais
ajaye atatoka kanda ya kaskazi kwa iyo yeye kama milya nini kilimuuthi na kama
aliuthika kwa nini na yeye asinge toa tamko lake badala ya kuhama chama ,na
alibainisha kuwa kiongozi huyu alipokuwa madarakani kwanini asiiseme ccm
na ubaya wake asubiri mpaka atoke ndani ya chama ndo aizungumzie hivyo
alisema kuwa hawa ndio watoto wa magamba na gamba kubwa linakuja nalo hawa
wanasafisha njia tu.
Aolibainisha kuwa Amefurahishwa na viongozi
hawa kujito katika chama kwani ndio wanafanya chama kiimarike zaidi kwani
kuondoka kwao kunasaida chama kujipanga upya na kuanza mapambano upya na
wanauhakika magamba yote yakitoka basi chama kitakuwa imara.
Alisema pia kutoka kwa wanachama hawa ni vizuri
kwani wanachama hawa walikasa wakabaini wao ndio wanaharibu chama hivyo
wameamua kujitoa ili wawaaachie watu wenye akili na mapenzi mema na chama
kukaa kukifanya chama kuwa kizuri na kipendwe na wananchi na wale
ambao walikuwa wamepoteza imani na chama basi wanaimani watarudi kwakuwa
wamegundua mafisadi na magamba yameshatoka.
“wakitoka chama kinakuwa kizuri kwani unajua
wananchi wanakipenda chama lakini wanakichukia kwa sababu ya viongozi wasiokuwa
waadilifu kwa iyo hawa wakiondoka na imani ata wananchi watarudisha imani na
chama chetu haswa wa mkoa wa Arusha.
Viongozi ambao wamejivua gamba na kukiama chama
cha mapinduzi mpaka sasa ni mwenyekiti UVCCM mkoa wa Arusha Jemsi Ole milya
,Diwani wa kata ya sombetini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi
Alfonce Mawazo pamoja na katibu mwenezi wa chama longido Yohane Laizer.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia