asilimia kubwa ya wanananchi wameshindwa kupiga kura kutokana na kuogopa wingi
wa maaskari waliokuwa wanazunguka katika jimbo la Arumeru mashariki pamoja na
wananchi wengi kutojua haki zao.
Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa uchaguzi Martina Kabisana wakati akiongea
na waandishi wa habari mara baada ya mgombea ubunge wa chadema Joshua Nassari
kutangazwa mshindi.
Alisema kuwa idadi kubwa ya wananchi wameshindwa kujitokeza kupiga kura
kutokana na kuwaogopa maaskari ambao walikuwa wengi wanazunguka zunguka katika
maeneo mbali mbali.
"unajua sio watu wote wapo sawa watu wengine wameshindwa kuja kupiga kura
mara baada ya kuona maaskari wengi wakiwa wanazunguka huku wakiwaa na mabomu
silaha hivyo wengine waliingia woga na ndomaana wakashidwa kuja kupiga
kura"alisema Kabisana
Alibainisha kuwambali na woga wa askari pia watu wengi wameshindwa kuja
kupiga kura kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya kupiga kura ,elimu ya
uraia pamoja na kutoelewa namna ya kutumia haki ya elimu ya kupiga kura.
Pia alibainisha kuwa kuna watu wengi pia ambao walipoteza shahada zao za
kupigia kura hivyo ndio sababu kubwa iliyofanya mpaka wananchi waliopiga kura
kuwa wachache kuliko wale ambao wamejiandikisha katika daftari la kudumu la
mpiga kura.
Aidha alibainisha kuwa zoezi lilienda vyema na wamemaliza salama ila alitoa
wito kwa tume ya uchaguzi kujitaidi kuelimisha wananchi kuhusiana na haki yake
ya kupiga kura na kuwahamasisha kutunza shahada zao za kupigia kura.
Jimbo hili la Arumeru mashariki lilikuwa na idadi ya wapiga kura 127455
lakini waliojitokeza kupiga kura ni wananchi 60699 tu katika jimbo hilo.