|
Timu ya JKT Oljoro ilijisahau mara
baada ya kushika nafasi nzuri wakati wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya
vodacom tanzania ndo ndio maana ikajibweteka.
hayo yamebainishwa na kocha msaidizi wa timu ya yanga Minjiro wakati
akiongwa na gazeti hili mara baada ya mechi yao kumalizika katika uwanja wa
kumbukumbu za sheikh amri abeid jijini arusha
Alisema kuwa timu ya Jkt Oljoro ni timu nzuri na inawachezaji wazuri ila
tatizo hawana uzoefu na na ligi kuiu pamoja kuwa walijipweteka mara baada ya
kumaliza mzunguko wa kwanza iliwezwa kuliswa mabao 4-1 katika uwanja wa
nyumbani.
katika mechi hii timu ya JKT oljoro ilionekana kuzidiwa nguvu katika
kipindi cha kwanza ambapo waliweza kufungwa magoli matatu kwa mfululizo ambapo
goli la kwaza liliweza kufungwa na mchezaji hamis Kiza kunako dakika ya 36
ambapo goli hili lilifungwa mara baada ya kupigwa kona na mchezaji Nurdin
Bakaari ,ambapo kanovaro alipokea na kumuunganiashia hamisi ambapo akufanya kosa
aliingiza mpira kimnyani.
Bao la pili liliingizwa kinyani na mchezaji Haruna Nionzima mchezajia
ambaye alionekana kuwakimbiza zaidii Jkt oljoro kunapo dakika ya 40 mara baada
ya kutokea shambulizi kali la piga ni pige ,mara baada ya bao hilo kuwekwa
kinyani mpira ulirudishwa kati na ilipotimu kunako dakika ya 44 mchezaji hamisi
kiza aliweza kuipatia timu yake bao ambalo liliipeleka mechi hii
mapumziko.
kipindi cha pili kilivyoanza timu ya jkt oljoro iliweza kujipatia baola
kufutia machozi kwa njia ya penati kupitia kwa mchezaji wao Hassani Othman
katika dakika 67 marabaada ya mchezaji Kanavaro kuunawa mpira.
mpira uliendelea chini ya muamuzi wa mechi hii martini Saanya kutoka
morogoro ambapo ilipotimu dakika ya 77 yanga waliweza kuongeza bao kupitia kwa
mchezaji hamisi kiza goli ambalo lilikataliwa kutokana na bao hilo kuingia
wakati mshika kibendera jesse Erasmo kunyosha bendera.
Yanga waliweza kujipatia goli la nne kunako dakika ya 84 kupitia kwa
mchezaji wao aliyefunga goli hilo kwa kisigino Pius Kisambale goli ambalo
liliwanyanyua mashabikii wa yanga kutoka majukwaani hadi katika viwanja kitu
ambacho kilimfanya muamuzi wa mechi hiyo kusimamisha mpira kwa muda usiopungua
dakika tano hadi pale polisi walipolazimika kuwasogeza mashabiki uwanjani na
mpira kuendelea.
hadi kipenga chamwisho kinalia timu ya
yanga ilikuwa unaongoza kwa mabao 4-1 LIBENEKE hili lilimtafuta kocha wa timu ya
Jkt Oljoro David Kulinga kuzungumzia swala hili naye alisema kuwa wamepokea
matokeo na wamekubaliana na hali ya mpira.