hichi ndicho kikosi cha simba SC
JIONI hii Simba SC
imeifunga Moro United mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, na sasa inahita pointi moja tu katika mechi zake tatu zilizobaki ili
kutawazwa rasmi kuwa mabingwa.
Simba wanawavua
ubingwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC ambao msimu huu ‘wamefulia’ kiasi cha
kukosa hata nafasi ya pili, ambayo ingewawezesha kucheza michuano yua Afrika
mwakani.
Hata hivyo mabigwa watetezi wa ligi kuu Yanga SC wanatarajia kuingia dimbani kuvaana na timu ya maafande wa JKT Oljoro jumatano hii katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid