Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusa mjini Godbless Lema katikati akiwa anatoka mahakamani mara baada ya ubunge wake kuenguliwa
Wannachi ambao ni wafuasi wa Chadema wakiwa wanamsubiri hukumu ya mbunge Lema
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema leo ameenguliwa nafasi yake ya ubunge mara ya Jaji mfadhiwidhi wa kanda ya sumbawanga Gabriel Rwakibalira kutangaza kuengua matokeo na hivyo sio mbunge tena kuanzia sasa.
Alisema kuwa hatua hiyo imefika mara baada ya kupitia vifungu vya sheria na kukuta lema alikiuka sheria za uchaguzi ,pamoja na kutoa lunga chafu katika mikutano yake aliyokuwa akifanya wakati wa kampeni.
Alisema kuwa katika mikutano ya lema aliyoifanya katika kipindi cha kampeni ambapo alifanya mikutano 60 na kati ya hivyo mikutano nane alikuwa akitoa lugha chafu .
kwa upande walema alisema kuwa hatakata rufaa na pia chama chake wapo tayari kurudia uchaguzi na anaimani watashinda