WANANACHI zaidi ya 300 wa kata za Maji ya Chai
na Maroroni wamevamia shamba lenye ukubwa wa zaidi ya Hekari6000lijulikanlo
kama Doll Estate lilopo katika kata ya Maji ya chai na kisha kuwavua nguo zote
walinzi huku wakiharibu mali
pamoja na kuiba vifaa mbalimbali vya wawekezaji hao.
Wakiongea na Waandishi wa habari mapema jana
Kiongozi wa idara ya wanyama katika shamba hilo Robson Peter alisema kuwa tukio lilitokea leo majira ya saa kumi nna moja za jioni ambapo wananchi hao walidai
kuwa shamba ni lao kama walivyoambiwa kwenye mikutano ya Kampeni na baadhi
ya Wagombea .
Aliendelea kusema kuwa wananchi hao ambao
walikuwa na silaha za jadi walivamia shamba hilo
ambalo linahusika na ufugaji wa wanyama mbalimbali kama vile Twiga,Swala,
Pundamilia ambapo walidai kuwa hawataki kuona wawekezaji wa kizungu ndani
ya shamba hilo
Walifafanua kuwa mara baada ya kuingia ndani ya
shamba hilo
huku tayari wakiwa wameshaaharibu na kuvunja ukuta wa zaidi ya kilomita nne
walimkamata Walinzi na kisha kumvua nguo zote huku wakimpa adhabu kali ambayo
ilimsababishia mlinzi huyo kutoweza kutoa taarifa
“walipoingia hapa majira hayo waliwavua nguo
walinzi waliokuwa zamu na kisha kuwapa adhabu huku wengine wakiendelea na
shuguli za uharibifu wa nyumba za hawa wawekeaji hali ambayo ilitufanya
tushindwe kupata msaada kwa wakati huo”aliongeza Bw Robson
Katika hatua nyingine alisema kuwa mara baada
ya watu hao kufanya vurugu hizo walilazimika kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi
kwa wilaya ya Meru ambapo Polisi walipofika waliwatanya wananchi hao kwa njia
ya mabomu.
Awali baadhi ya wawekezaji katika shamba hilo ambao hawakupenda kutajwa majina yao
hadharani walisema kuwa walichokifanya wananchi wa kata hizo hasa kijiji cha
Kitefu si cha uungwana kabisa kwa kuwa mpaka sasa wanaishi kwa ushirikiano
mkubwa sana
Wawekezaji hao walisema wapo kwenye shamba hilo kwa mujibu wa sheria za uwekezaji wan chi ya Tanzania na
tayari mpaka sasa wameshawekeana mipango na mikakati mbalimbali ya ushirikiano
dhdii ya wananchi hao
“tunashangaa sana wanakijiji wa hapa wanaposema
kuwa hawataki kutuona wakati sisi tuna haki kisheria na pia kama ni wananchi
kunufaika na sisi mbona tuna mikakati mikubwa sana na wote wanajua kila
kinachoendelea lakini leo wamevuja nyumba zetu na kuchukua mali zetu
hatujapendezwa na hali hiii hata kidogo”walisema wawekezaji hao
Hataivyo baadhi ya wananchi wa kata hiyo
walisema kuwa kuvamiwa kwa wawekezaji hao kunatokaa na kauli za siasa
hasa za kampeni na viongozi mbalimbali hali ambayo mpaka sasa
imepandika mbegu chafu kwenye jimbo hilo
dhidi ya wawekezaji mbalimbali
“juzi viongozi wa vyama viwili ambavyo vilikuwa
vinachuana walidai kuwa haya mashamba ni mali
ya wananchi chama hicho walidai kuwa wananchi, nao wananchi waliposubuiri
uchaguzi uishe waakaamua kuingia ili wachukue mashamba yao lakini kwa hili inabidi nguvu za ziada
zitumike kwa kuwa hawa wao sawa kisheria”walisema wananchi hao
Naye diwani wa kata ya Maji Loti Nnko alidhibitisha kutokea kwa uharibifu
wa mali za wawekezaji hao ambapo alidai kuwa mpaka sasa thamani halisi bado
haijapatikana Wakati Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye naye alikiri kuwepo kwa
tukio hilo ila bado jeshi la Polisi linaendelea na utaratibu wake