UVCCM ARUSHA WAMVAA OLE MILYA

 wa kwanza kulia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa Salome Khatibu akimjumbe fua tiwa wa kwanza kulia ni Kenedy Mpumilwa
mjumbe wa baraza kuu la vijana ccm taifa muwakillishi wa mkoa wa Arusha ,ambaye pia ni katibu uchumi miradi na fedha mkoa wa Arusha Mrisho gambo akiwae anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na kudaiwa kwa milya


WIMBI la viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhama na
kujiunga na Chama ha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), sasa imeanza
kukitikisa chama hicho tawala na kuamua kumshambulia aliyekuwa
Mwenyekiti wa UVCCM, mkoa wa Arusha, James Ole Millya aliyeuanzisha
kuwa amekimbia na milioni mbili zililenga kuanzisha Saccos ya vijana
Arusha.

Pamoja na kumtuhumu Ole Millya kwa kuondoka na fedha hizo zilizotolewa
na waliokuwa wabunge wa jimbo la Arusha mjini, Felix Mrema na Arumeru
Magharibi, Elisa Mollel mwaka 2008, CCM pia inadai aliyekuwa Menyekiti
huyo wa vijana hajakabidhi taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi
cha miaka mitatu liyopita inayokadiriwa kufikia milioni 600.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mjumbe wa
Baraza Kuu la UVCCM Taifa anayewakilisha mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
na Mjumbe wa Baraza la vijana mkoa wa Arusha, Kennedy Mpumilwa
walimrushia madongo Ole Millya kwa kumita msumari iliyokuwa ukitoboa
tairi la gari (CCM) na kusababisha lipate pancha.

“Kwa ujumla vijana Arusha tumefurahishwa na kitendo cha Ole Millya
kuhama kwani alikuwa akikidhoofisha chama badala ya kukijenga kwa
kuanzisha vurugu zilizosababisha mpasuko mkubwa mkoani Arusha, alikuwa
msumari iliyokuwa kitoboa tairi la gari letu na kusababisha lipate
pancha alilodai kumfanya ahame,” alisema Gambo

Gambo ambaye ni mpinzani mkubwa wa Ole Millya ambao ugomvi wao
ulisababisha waadhibiwe kwa kupewa ono kali na kikao cha halmashauri
ya CCM mkoa wa Arusha mwishoni mwa mwaka uliopita alielezea kitendo
cha aliyekuwa Mwenyekiti wake huyo kuhamia Chadema kama dalili njema
kuwa kwa utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba aliyoasisiwa na
Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete Februari, mwaka jana.

Alimfananisha Ole Millya na wengine waliotangaza kujivua uanachama wa
CCM na kjiunga Chadema na magamba dagaa ambao wanapalilia njia kwa
magamba wakubwa kufuata.

“Pamoja na kuhama na kupokewa kwa shangwe na Chadema, vijana wa CCM
Arusha tutaendelea kumdai Millya milioni 2 zetu zilizolenga kuanzisha
Saccos ambazo hajazikabidhi tangu alipokabidhiwa mwaka 2008. Tutamdai
yeye akiwa hai au mfu na asipolipa tutaendelea kudai watoto wake hadi
wajukuu,” alisema Gambo.

Akijibu swali kwanini wanajitokeza kudai fedha hizo karibia miaka sita
sasa tangu zitolewe, hasa kipindi hiki ambacho Ole Millya amejitoa CCM
na kuhamia Chadema,
Gambo alidai mara nyingi vikao vya kuzungumzia suala hilo vimekuwa
vikivunjika bila muafaka kupatikana kutokana na vurugu zinazoanzishwa
na wapambe wa aliyekuwa mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake, Mpumilwa alidai Ole Millya ameondoka bila kutoa
mapato na matumizi ya zaidi ya milioni 600 zilizopatikana kutokana na
pango inayolipwa na wafanyabiashara na wenye maofisi katika vyumba 96
vya biashara vinavyomilikiwa na UVCCM vinavyopangishwa kwa wastani wa
shilingi 150,000 hadi 300,000 kwa mwezi.

Mwana CCM mwingine aliyehudhuria mkutano huo aliyejitambulisha kama
mjumbe mstaafu wa Baraza la vijana wa CCM mkoa wa Arusha, Salome
Hatibu alitoa changamoto kwa Chadema kumkabidhi Ole Millya moja ya
wilaya za mkoa wa Arusha kuhamasisha ujenzi wa chama chake kipya ili
kuthibitisha iwapo anaungwa mkono na vijana na wanachama wa chama
hicho tawala kama alivyoeleza alipotangaza kujivua uanachama na kudai
wengi watamfuata.

Akizungumzia tuhuma zilizoelekezwa dhidi yake kwa njia ya simu jana,
Ole Millya alisema ni dalili za kuanza kuchanganyikiwa kwani kwa uwezo
wake kiuchumi hawezi kuchukua hata senti moja ya chama bali alikuwa
akitumia fedha zake binafsi kutekeleza baadhi ya majukumu ya kukijenga
CCM.

“Lakini jambo kubwa la kujiuliza ni je, fedha za Jumuiya zinapokelewa
na kuhifadhiwa na Mwenyekiti? Je, Mwenyekiti ni returning officer wa
UVCCM hadi mimi nihojiwe kuhusu fedha za mapato na matumizi ya
Jumuiya?” alisema na kuhoji Ole Millya.

Wakati viongozi na wana CCM hao mkoani Arusha na wengine wa ngazi ya
kitaifa wakimponda Ole Millya na kufikia kumwita mzigo au gamba,
tayari watu kadhaa wametangaza kujitoa CCM na kujiunga Chadema
kumuunga mkono mwenyekiti huyo wa zamani wa UVCCM.

Miongoni mwa waliojitoa CCM na kujiunga Chadema wamo madiwani kutoka
Manispaa ya Arusha na halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza
pamoja na wenyeviti wa serikali za mtaa wilayani Ngorongoro
walioondoka na wananchi zaidi ya 2,500 huku wengi wakiahidi kufuata
kwa kile kinachoelezwa kuchoshwa na ubabaishaji ndani ya chama hicho
tawala.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post