Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na maraisi wenzake wakitia saini mkataba wa ulinzi wa nchi hizo
Wakuu wa wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki wakionyesha hati baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo
Wakuu wa wanchi wanachama wa jumuiya wakiwa katika picha ya pamoja
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) wanatarajiwa kukutana Arusha, Tanzania hii leo, katika mkutano
maalum utakaojadili pamoja na mambo mengine, mapendekezo ya
maombi
ya nchi ya Sudan Kusini, kujiunga na jumuiya hiyo.
Nchi
zote tano za Kenya, Uganda, Tanzania,Rwanda na Burundi zinatarajiwa kuhudhuria
mkutano huo wa siku moja utakaofanyika katika hoteli ya Ngurdoto, nje kidogo ya
mji wa Arusha.
Taarifa
zilizopatikana toka ofisi ya EAC,Idara ya Mawasiliano na Masuala ya Umma imesema
mkutano huo pia unatarajiwa kujadili agenda nyingine nne.
Maombi
ya Sudani Kusini yatafikiriwa ikiwa ni miezi karibu mitano baada ya maombi ya
Jamhuri ya Sudani kukataliwa kwa madai ya kutokidhi vigezo vilivyoanzisha
mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkataba
huo unaeleza wazi kwamba nchi yoyote inayotaka kujiunga na EAC, sharti iwe
imepakana na moja kati ya nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo.
Hata
hivyo maombi ya Sudani Kusini yanakuja wakati ambapo ipo katika hali ya
uwezekano wa kuingia katika vita kamili na jirani yake, Sudani Kaskazini, hoja
ambayo huenda pia itatupiwa jicho na kikao hicho cha Wakuu wa EAC.
Nchi
hiyo mpya kabisa barani Afrika na duniani kwa ujumla, ilipatikana Julai 1, 2011
baada ya mwongo mmoja wa vita na Sudani Kaskazini.
Hoja
nyingine ambazo zinatarajiwa pia kujadilia katika mkutano huo ni pamoja na
uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu mpya wa EAC, atakayeshughulikia Shirikisho la
Kisiasa, kuchukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Beatrice Kiraso wa Uganda
ambaye kamaliza mkataba wake wa kazi na pia kufikiria kumwongezea mkataba wa
kazi, Naibu Katibu Mkuu, anayeshughulikia Uzalishaji na Sekta ya Jamii, Jean
Claude Nsengiyumva kutoka Burundi.
Mkutano
huo wa Wakuu wa EAC, umetanguliwa na mkutano maalum wa 24 wa Baraza la Mawaziri
wa EAC.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia