MGOGORO mkubwa umeibuka baina ya wananchi
na viongozi wa kata ya baraa,jijini Arusha ambapo wananchi hao wameamua
kujichukulia sheria mkononi kwa kubomoa nyumba mbalimbali zilizojengwa kwenye
maeneo ya wazi .
Wananchi hao wakiwa na jazba
wameadhimia kubomoa nyumba zote zilizojengwa kinyume cha sheria
,kwenye maeneo ya wazi likiwemo jengo la chuo cha ualimu cha Silla,huku
wakiwatuhumu viongozi wa kata hiyo akiwemo diwani,Lotti Laizer kuuza maeneo ya
wazi.
Wamedai kuwa viongozi wa mitaa
akiwemo mwenyeviti wa mtaa wa kwa mrefu,Godson Melejack(Kamili) na mwenyekiti wa
mtaa wa Sorenyi ,Estomy Taretoi , wamekuwa wakishirikiana na diwani wa kata hiyo
Loti Laizer kumega eneo la wazi lenye ukubwa wa zaidi ya ekali nane na kuliuza
kidogo kidogo kwa nyakati tofauti kwa wafanyabiashara na wakazi
.
Katika utekelezaji wa zoezi la
uvunjaji nyumba hizo lililofanyiaka alfajiri ya leo ,kuliibuka vurugu kubwa
baina ya wananchi hao na wamiliki wa nyumba hizo kiasi cha kuwalazimu viongozi
wa mitaa ya kata hiyo kufika eneo hilo na kukubaliana kufanyika kwa kikao cha
pamoja ,Mai 3 mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
George Elphas mkazi wa kata hiyo alisema kuwa tangu mwaka 2003 kumekuwepo na
mgogoro wa Ardhi katika kata hiyo ,na kwamba mgogoro huo umekuwa
ukisababishwa na na viongozi wa kata hiyo wasio waaminifu akiwemo diwani Laizer
ambaye wamemtuhumu kuwarubuni viongozi wa kata na wenyeviti wa mtaa katika
kuifanikisha uuzaji wa maeneo nya wazi.
Wamemtuhumu diwani Laizer kwamba
amekuwa na nguvu ya kutoa ushawishi kwa kila kiongozi anayehamia kufanya kazi
katika kata hiyo na kusababisha maeneo hayo kuuzwa bila woga.
Alisema kuwa wamechoshwa na vitendo
vya udhalimu vinavyofanywa na viongozi wao kwani wamejaribu kulalamika ngazi
mbalimbali lakini wamekuwa hawapati ushirikiano ila kwa sasa wamedhamilia kuanza
kuvunja nyumba zote zilizojengwa ndani ya eneo la wazi.
Nae mkazi mwingine ,Amos Godson
amedai kuwa eneo ni muhimu sana kwa maendeleo ya kata hiyo kwa walikua na mpango
wa kuliendeleza kwa kujenga shule,dhahanati pamoja na huduma zingine muhimu kwa
wananchi.
Wananchi hao tayari wameanza kuvunja
baadhi ya nyumba hali iliyozua mtafaluku mkubwa baina ya wenye nyumba pamoja na
viongozi hao ambao walinusulika kupigwa baada ya wananchi hao kupandwa na jazba
wakiwatuhumu kujineemesha na maeneo yawazi.
Hata hivyo wananchi hao wamepanga
kuvunja jengo la chuo cha ualimu cha Silla kilichopo katika kata
hiyo ambapo mmiliki wake alinunua eneo la hilo la wazi na kuamua kujenga chuo
hilo ili hali alikuwa na taarifa kuwa ni eneo la wazi nba kuamua kujenga chuo
hicho bila kujali kelele za wananchi.
Akizungumzia sakata hilo diwani wa
kata hiyo, Lotti Laiser alisema kuwa yeye kuhusishwa na tuhumu hizo ni jambo
ambalo halimwingii akilini ,kwani muda mwingi amekuwa akishiriki kuhakikisha
kuwa eneo hilo haliuzwi.
Alifafanua kuwa yeye ndiye
aliyehusika kutafuta askaripolisi kwa lengo la kumkamata mtu anayejenga usiku
ndani ya eneo hilo la wazi na kudai kuwa ,ameshtushwa na yeye kuhusishwa na
tuhuma uuzwaji wa eneo hilo..
''Nasema kuwa mimi sihusiki na lolote
juu ya tuhuma hizo ninachokuomba chukua jina ya mtu anayenituhumu ili baadae
nimkamate na kumweka ndani athibitishe madai yake ,sina njaa ya aina
hiyo''alisema Laiser kwa njia ya simu alipokuwa akihojiwa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia