BREAKING NEWS

Monday, April 23, 2012

WAVAMIA SHAMBA LA MUWEKEZAJI

Wananchi wakazi wa Machumba kata ya Nkwandua wilayani Arumeru  wamevamia shamba la mwekezaji linalofahamika kama Mashumba estate na kujigawia ardhi kwa madai kuwa wanafanywa watumwa kwenye nchi yao huku wakuja wakijitwalia maeneo na kufaidi rasilimali za nchi hii.

Wakazi hao wamavamia mashamba hayo yenye ukubwa wa hekari 400 saa 9 usiku wa kuamikia leo na kujigawia ardhi hiyo wakidai kuwa wanacheweshwa kupata ridhiki zao licha kuwa serekali ikwisha waambia kuwa wafanyesubra ilikulitatua tatizo la ardhi na mwekezaji huyo aliekimbia usiku wa leo.

Makundi ya vijana na kinamama walikuwa wakigawana ardhi ya shamba hilo huku wakisema sasa ndiyo mwisho wamafisadi kwani tumechoka kugandamizwa na kuwa watumwa katika nchi yetu ardhi yetu ya muhindi.

Walidai kuwa mzee Kirilo alikwenda UN kudai haki ya weusi kumiliki mashamba (Ardhi) lakini mashamba makubwa yanamilikiwa na wenye hela wakati maskini tunaendela kutizama katika nchi yetu sasa tunasema basi kama kufia hapa alisema alfred Akyoo

Akyo alisema kuwa njia yakwenda vijiji vya kusini hadi chekereni lazima uzunguke shangarai na ukienda makusaro lazima uende Tengeru haya mashamba yamezuia njia zote na serekali haina la kusema njia nyepesi ni lazima upite katikati ya mashamba hayo

"Leo usiku vijana wa singi'si woanaenda kuvamia mashamba ya Sadc na baadae mashamba ya Gomba ESTATE katika muendelezo huo wa kudai haki zetu na kwa hili watatuulia hapa hakuna kulala hadi kieleweke" alisema akyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo limetokea kweli na jeshi la polisi lilazimika kuwatawanya watu hao kwa kutumia mabomu ya machozi na kubainishakuwa hakuna ata mtu mmoja alieshikiliwa kutokana na tukio hilo

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates