Vijana wa chama cha demokrasia
namaendeleo Chadema wameweza kukusanyika kwa wingi katika kituo cha kata ya
king'ori wakiwa wanashinikiza kupatiwa matokeo ya uchaguzi katika kata
yao.
Hayo yametokea mara baada ya wasimamizi wa kituo hicho kuchelewa kubandika
matokeo ya uchaguzi ambapo mpaka ilipotimu mnamo majira ya saa moja kamili ya
usiku matokeo hayo yaolikuwa hayabandikwa
Nipishe iliweza kushuhudia baadhi ya viongozi wa chama cha chadema wakiwa
wanawatuliza wafuasi wao huku askari waliokuwa katika vituo hivi wakiwasihi
vijana hao kuacha fujo na kusubiri kura zimaliizwe kuhesabiwa ndipo wapewe
matokeo yao ,kitu ambacho vijana hao walikubali kutulia kwa muda wakiwa
wanasubiri matokeo yao huku wakiimba nyimbo mbalimbali za vyama vyao pamoja na
kuimba nyimbo tunataka matokeo msipo tupa tunawavamia .
Kitondo hicho cha vijana hao kuimba kiliendelea hadi matukeo hayo
yalivyobandikwa na wananchi wakayasoma nakuondoka .
katika vituo mbalimbali vya kata ya king'ori chadema na ccm iliweza
kuendana sawa huku sehemu nyingine Ccm ikionyesha kushinda na sehemu nyingine
Chadema kushinda na baadhi ya sehemu kutoka sare
katika baadhi ya vituo ambavyo nipashe
imeweza kupata matokeo hadi sasa ni pamoja na kituo hicho cha kata ya King'ori
jengo la chama ambapo kituo cha kwanza CCM waliongoza kwa kura 117 huku chadema
wakwa na kura 116 ,AFP kkura 1,UPDP hawajapata kitu DP kura moja huku kura mbili
zikiwazimeharibika
katika kituo cha pilicha kata ya king'ori CCM wameongoza kwa kura 129 huku
chadema wakiwa na kura 105 ,AFP wakiwa na kura moja,UPDP wakiwa wameambulia kura
moja zilizoharibika ikiwa ni kura moja
Kwa upande wa kituo cha tatu cha Kingori kata CCM wameongoza kwa kura 125
,chadema kura 110 huku kura zilizoharibika zikiwa ni jumla ya kura sita,katika
kituo cha nne Chadema wameweza kuongoza kwa kura 126 huku ccm wakiwa wanakura
86 na katika kura zilizoharibika hamna.
katika kituo cha zahanati Chadema wameweza kuongoza katika kituo cha kwa
kwa kupata kura 196 huku ccm wakiwa na kura 143 zilizoharibika zikiwa ni kura
tatu,huku kituo cha pili zahanati CCM wakiwa wanaongoza kwa kura137 na chadema
wakiwa na kura 102 na zilizoharibika zikiwa ni kura mbili.
nacho kituo cha Ghala la mazao Malula chadema waliweza kuongoza kwa kura 87
huku CCM
wakiwa na kura 48,na katika kituo cha
pili cha Ghala la mazao Malula Chadema waliweza kuongoza kwa kura 83huku CCM
wakiwa na kura 37 na kupande wa kituo cha tatu Chadema pia walioweza kuongoza
kwa kura 70 huku CCM wakiwa na kura 68,katika kituo cha shule ya msingi
kwatulele Chadema pia wameweza kuongoza kwa kura 68 huku CCM wakiwa na kura
58,na kituo cha pili cha Shule ya Msingi Kwatulele Chadema pia wameongoza kwa
kura 74 huku CCM wakiwa na kura 69 wakati chama cha DP kikiwa kimepata kura
moja.
Kwa upande wa kituo cha tatu cha shule ya msingi kwatulele chadema na ccm
wameweza kufungana mara baada ya kupata kura sawa kwa sawa wote wakiwa na kura
72 kila mmoja.
katika kituo kingine cha shule ya msingi Mikuni CCM waliweza kuongoza
kwakura 87 huku chadema wakiwa na kura 72 na kwa upande wa kituo cha pili cha
shule ya Msingi mikuni CCM pia waliongoza kwa kuraa 100 huku chadema wakiwa na
kura 61
kwa upande wa kituo cha Akeri kituo cha kwandua CCMimepata kura 60 chadema 192,kituo kingine cha pili CCM 116 na chadema wamepata 166, kituo kingine 94 chadema ccm 88 Kituo cha shule Akeri Chadema wamepata kura 46 CCM 250 .
Kwa sasa katika maeneo ya leganga,usa river,Tengeru mabomu yanaendelea kwa wingi kila mahala na kuna baadhi ya wananchi wameumizwa lakini libeneke alijabaini ni nini kimewaumiza