TAMKO RASMI LA CHADEMA TUTATOA JUMAMOSI

kamanda akisakata rumba nje ya ofisi za chadema wakati wakimngoja mwenyekiti wa chama



 Mwenyekiti Freeman Mbowe akiwa anaongea na wananchi wa Arusha nje ya ofisi ya mkoa ya Chadema
wananchi ambao ni wafuasi wa chadema wakiwa wanamsikiliza mwenyekiti wa Chadema akihutubia


mwenyekiti wa C hadema Freeman Mbowe katikati kulia ni mbunge mteule wa jimbo la Arumeru Mashariki ,kushoto ni mbune aliye enguliwa Godbless Lema wakati mwenyekiti akiongea nje ya ofisi ya chama kuhusiana na kuenguliwa kwa mbunge

MAHAKAMA KUU
KANDA YA ARUSHA


Mahakama kuu Mkoa wa Arusha imetengua matokeo ya Ubunge wa Jimbo la
Arusha Mjini ambalo lilikuwa chini ya Bw Goodbless Lema mara baada ya
kukutwa na hatia ya kukiukia maadili wakati wa kampeni za uchaguzi za
mwaka 2010.

Akitoa hukumu hiyo katika mahakama hiyo Jaji kutoka mahakama ya kanda
ya Sumbawanga Jaji Mfawidhi Bw Gabriel Rwakibarira alisema kuwa katika
malalamiko 10 yaliyopelekwa na wafuasi wa chama cha mapinduzi (CCM)
Mbunge Lema alikutwa na hatia

Jaji huyo alisema kuwa katika mikutano 60 ya kampeni ambayo alifanya
Bw Lema Mikutano 8 alikiuka maadili kinyume cha sheria na taratibu za
uchaguzi jambo ambalo linafanya matokeo yake ya Ubunge yatenguliwe

Alisema kuwa ndani ya malalamkiko hayo kumi ambayo yamewasilishwa
mahakamani hapo alikutwa na hatia katika makosa 8 ambapo mawili
hayakukubalika kwa mujibu wa sheria na taratibu za mahakama

“kwa mujibu wa sheria na taratibu Lema amekutwa na hatia katika
malalamikio na dondoo nane kwa hali hiyo nasema kuwa nabatilisha
matokeo ya ubunge wa jimbo la Arusha Mjini na kwa hali hiyo taratibu
nyingine zinatakiwa kuanza kufuatwa “aliongeza Jaji Gabriel

Pia alifafanua kuwa kwa mujibu wa sheria namba 114 katika kifungu
kidogo cha kwanza hadi cha saba cha sheria za uchaguzi msajili wa
mahakama kwa kanda ya Arusha anatakiwa kukitumia kwa kuhakikisha kuwa
anapeleka taarifa kwa tume ya uchaguzi juu ya kunbatilishwwa kwa
matokeo hayo

“Msajili wa mahakama anatakiwa kutumia kifungu hiki na kuhakikisha
kuwa tume inakuwa huru kwa kuwa mpaka sasa tayari mahakama
imeshatengua matokeo kwa mujibu wa sheria za mahakama”aliongeza Jaji
Gabriel

Hataivyo alisema kuwa bado Mbunge huyo ana nafasi ya kukata rufaa
kwenye ngazi za juu za mahakama endapo kama hataridhika na mnwenendo
wa kesi pamoja na hukumu ambayo iliyotolewa ndani ya mahakama hiyo
kwa muda wa siku 30.

Naye Bw Lema alisema kuwa pamoja na kutenguliwa kwake kwa ubunge wa
jimbo la Arusha mjini bado yeye ndiye ,mbunge na hata kama uchaguzi
utarudiwa ni wazi kuwa yeye ndiye atakayeshinda ingawaje hizo ni Mbinu
za Viongozi wa juu Taifa la Tanzania (MAJINA TUNAYO)ambazo toka hapo
awali alikuwa amezikataa.

Bw Lema aliongeza kuwa Mahakama kupitia kesi yake imeonesha wazi jinsi
ambavyo wanavyobaka Demokrasia na suala hilo litawapeleka watu katika
misitu bila kupenda na pia nchi itaingia katika machafuko.

Alifafanua kuwa mpaka sasa yeye ni jasiri wa hali ya juu sana na kwa
hali hiyo atahakikisha kuwa anapambana kwa nguvu zote katika kutetea
haki za wanyonge hata kama ametenguliwa ubunge wa Arusha Mjini.

“ninachoweza kusema ni kuwa nina moyo mkubwa sana kwani mimi nimepita
katika mapito ya hali ya juu sana na pia aliyeniweka madarakani ni
Mungu na wala sio hao viongozi wa ngazi za juu na ninapenda kuwatia
moyo kuwa hii hukumu ya kutengenezwa kama siyo ya kutengenezwa
imekuwwaje kilakiongozi anajua hii hukumu kuanzia juzi na
jana”alisema Bw Lema

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
Bw Freeman Mbowe alisema kuwa hiki ni kipindi kigumu sana kwao na pia
ni kipindi cha mpito, pamoja na kuweka jazba pembeni badala yake
chama hicho kinatakiwa kuonesha dunia , mahakama jinsi haki
inavyopatikana

Bw Mbowe alisema kuwa chama hicho hakiwezi kukataa ama kukuabali
hukumu ya mahakama badala yake chama hicho kinalenga kutafuta haki
siku ya Jumamosi katika viwanja vya NMC jijini hapa ambapo pia
watashahuriana kabla na kasha kutoa tamko.

“Mimi naheshimu sana mahakama kwa kuwa inataratibu zake za msingi na
kwa hali hiyo nawasihi sana wananchi kuwa watulivu kwa siku hizi mbili
mpaka jumamosi tutatoa hatma yetu kama tutakata rufaa au laa na baada
ya kushahuriana na viongozi na wanasheria wetu wa chama “aliongeza Bw
Mbowe

Kwa upande wa walalamikaji,ambaye aliongea kwa niaba ya wenzake Bw
Happy Kivuyo alisema kuwa mahakama imefanya uamuzi wa hali ya juu sana
na imeonesha haki kwa kuwa Bw lema alikuwa anatoa lugha za matusi na
kuzalilisha sana

Bw Happy alisema kuwa wao walichokuwa wanakitaka ni haki na wala sio
Ubunge kwa kuwa hilo litakuwa ni funmdisho hata kwa wagombea wengine
ambao wanazalilisha watu kijinsia kwa madai kuwa wapo kwenye Kampeni

“Napenda niwaambie wakazi wa mji wa Arusha kuwa malalamiko yetu
hayakuwa ya kuchonga ila yalikuwa ni ya msingi wa hali ya juu sana na
kwa hali hiyo mahakama imefanya uamuzi wa hali ya juu sana”alisema Bw
Happy

Hataivyo mara baada ya hukumu hiyo shuguli za mahakama zilifungwa huku
kila kona ya jiji ikilindwa na Polisi wa kuzuia vurugu,huku shuguli
mbalimbali za maendeleo zikisimama kwa muda kutokana na wingi wa watu

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post