Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la moja la Seleman ambaye
ni dereva wa piki piki amefariki dunia mara baada ya piki piki yake kugongana uso kwa uso na gari
aina ya Mitsubishi fuso
Akithibitisha kutoka kwa tukio hilo
kamanda wa polisi mkoani Ausha Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea April 18 majira ya saa 3:00 asubuhi katika
barabara ya dodoma
maeneo ya Jumbo ndani ya halmashauri ya jiji la arusha .
Alisema kuwa gari
aina ya Mitsubishi fuso yenye namba za usajili T.586 ATV lililokuwa likisendeshwa
na Paulo Kiloli (26)mkazi wa mbauda liligongana na piki piki aina ya toyo yenye
namba ya usajili T.514 BWZ iliyokuwa inaendeshwa na marehemu.
Alisma kuwa ajali hiyo alitokea wakati wakati vyombo hivyo vya
usafiri vikiwa katika uelekeo mmoja toka maeneo ya kisongo kuelekea maeneo ya kilombero
lakini walipofika maeneo hayo dereva wa piki piki alijaribu kulipita gari hilo kupitia upande wa kushoto
hivyo kubabisha kutokea kwa ajali hiyo
Andengenye alisema kuwa jeshi la polisi mkoani hapa lilifanikiwa
kumkamata dereva wa gari hilo
na anaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi utakapokamilika na kubainika alikuwa nakosa basi atafikishwa mahakamani
na mwili wa marehemu Seleman umeifadhiwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha hospitali
ya mkoa ya maunti meru.