HOSPITALI ya
Seliani iliyopo mkoani hapa imetoa msaada wa madawa kwa wagonjwa zaidiya 50
wenye magonjwa sugu katika kanisa la KKKT usharika wa Ilboru.
Akikabidhi misaada
hiyo kwa wagonjwa hao mhudumu wa Hocpiece/Home based care kutoka hospitali hiyo
bw Emanueli Abrahamu alisema kuwa jamii inatakiwa kujitokeza na kuwatia moyo
wasiojiweza ili wasijione wametengwa .
Aidha alisema kuwa
watanzania wanatakiwa kuacha kuwanyanyapaa wagonjwa kwa kuwanyima haki zao za
msingi na badala yake wawapatie misaada na kuwatia moyo ili wazidi
kuishi kwa matumaini.
Vile vile aliwaasa
wagonjwa kuacha kujinyanyapaa kwani unyanyapaa huondoa utu wa mtu ambapo
unyanyapaa mojawapo ni pamoja na kuacha masharti ya utumiaji wa madawa na
kutokuhudhuria sehemu zinazotolewa misaada .
Nae bw Elphas
Thomas ambaye ni mwinjilisti wa kanisa hilo alisema kuwa wagonjwa ambao
wamepatiwa misaada huo wa madawa ya kupunguza makali ni wale
wenye magonjwa kama vile kansa,ukimwi na tb.
Aidha alieleza
kuwa misaada mingine iliyotolewa kwa wagonjwa hao ni pamoja na
nguo,vyakula,na matunda ambapo pia huduma hiyo inategemea kuwahudumia wagonjwa
zaidi ya elfu tatu na mia sita ambao wapo majumbani.
Hata hivyo
wagonjwa hao waliopatiwa misaada hiyo waliishukuru taasisi ya selian kwa
kuwapatia msaada huo nna kusema kuwa watakuwa wajumbe wa kuwashauri kwenda
kupima afya zao ili kupunguza maambukizi ya magonjwa hayo sugu.